Mama Ursula alitangazwa mtakatifu na Baba Mtakatifu Johani Paulo II huko Roma 18.V.2003 |
Ursuline Sisters P. O. Box 96 Itigi - Mkiwa Singida |
ROHO YA SHIRIKA Mursula kwa wito wake anajiunganisha kwa namna ya pekee na Fumbo la Mateso ya Kristo ambaye akitumwa na Baba, aliwapenda hivyo wanadamu hata kujitoa mwenyewe kama sadaka kwa njia ya kifo chake msalabani. Kwa njia ya mateso yake wanadamu wote washiriki kifo chake na ufufuko wake, ili waufikie uzima wa milele. Masista wanajaribu kuitikia neno la Kristu: “Ninaona kiu” wakijitolea mhanga kikamilifu kwa upendo wa Moyo wa Yesu, pasipo kiasi, wakishirikiana kwa ajili ya wokovu wa wanadamu.
Kielelezo cha maisha ya masista waursula ni maneno ya Bikira Maria aliyomjibu malaika: „Tazama mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena” . Maneno haya ni „motto” wa waursula wa Moyo Mtakatifu wa Yesu Mteswa.
|
KARAMA Utume wa pekee wa Shirika ndani ya Kanisa ni: „Kumtangaza Kristo, Upendo wa Moyo wake, kwa njia ya malezi na elimu kwa watoto na vijana, huduma kwa ndugu walio wahitaji sana na wanaodhulumiwa na pia kwa njia ya amali nyingine katika uwanja wa mahubiri ya Injili kwa ulimwengu” (Katiba 1987)
Mtakatifu Anjela Merici (1474 – 1540)
|
MISIONI YA TANZANIA |
MAKTABA
"Pendekezo kwa ajili yako..." - sista Rita Fiorillo "Furaha ya Mama Ursula" - Tafakari ya p.Carlo Calori "Maisha ya Mt. Ursula" - p. Richard Mjigwa CPPS
|
MAANDISHI
|