Masista wa UrsulaESPANSIONE-descrizione in lingua italianaTanzania

 

    MAMA URSULA GIULIA LEDOCHOWSKA alizaliwa mwaka 1865 huko Loosdorf karibu na Vienna. Baba yake Antoni Ledochowski alikuwa mzaliwa wa Polonia. Mama yake Josefina Salis Zizers alikuwa mkaaji wa Stwitzland.


    Dada yake mkubwa Maria Teresia Mwanzilishi wa Wamisionari wa Mt.Petro Claver aliitwa mwenye Heri mwaka 1975. Kaka yake mdogo Vladimiro, alikuwa kwa miaka mingi Mkuu wa WaYesuiti.

    Kwenye miaka 21 Giulia aliingia Shirikani kwa wa Ursula wa Cracovia.

Utume wake wa kitume na kuelimisha alianza mwaka 1907 huko Russia na Finlandia, wakati ule ikiambatana na Russia.

    Alifukuzwa mwake 1914 akakimbilia Svezia na Danimarca. Alitambua kwa kuona kwa undani, utume na bidii ya kutochoka kwa kutetea usawa wa heshina wa mwanadamu. Alikuwa na kipaji maalum kilichomfanya aweze kuwaunganisha watu mbali mbali na fikra katika wazo kwa mfano kuchukua msaada kwa majeruhi ya vita vya kwanza vya dunia, kwa njia kufanya mikutano na kwa mazungumzo. Katika mwaka 1920 alirudi Polonia ambapo kwa ruhusa ya Santa Sede, aliunda tawi jipya la wa-Ursula: "Wa-Ursula wa Moyo wa Yesu Mteswa" ambao lengo lao la kwanza ni kusaidia vijana wenye kuhitaji msaada, tena wako tayari kwa mahitaji ya kiroho na ya kimwili ya kila nchi na kila mazingira. Kwa kuona sana uhitaji wa watu alikuwa hodari kwa kuvumbua njia mpya kwa maisha ya kitawa kwa kuelimisha, kwa kazi ya kitume na kwa hekima kwa wote.

            Alikufa Roma mwaka 1939.


Mama Ursula atitangazwa mwenye heri na Baba Mtakatifu Johani Paulo II

huko Poznan-Polonia tarehe 20.VI.1983


Mama Ursula alitangazwa mtakatifu na Baba Mtakatifu Johani Paulo II huko Roma 18.V.2003