Jubilei ya miaka 150 tangu alipozaliwa
Mtakatifu Ursula 1865-1939
Katika
mwaka huu wa jubilei, tunataka, awali ya yote, kumshukuru Mungu kwa ajili ya
zawadi ya Mtakatifu Ursula, aliyotoa sio tu kwa Shirika letu, bali hata kwa
Kanisa zima na dunia.
Kwa mpango na kwa Maongozi ya Mungu, maadhimisho ya miaka 150 ya kuzaliwa kwa
Mtakatifu Ursula, yako katika Mwaka wa Watawa. Wakati wa maadhimisho mengi
yanayopangwa kufanyika sehemu mbalimbali za dunia ambapo sisi tunaishi na
kufanya kazi, tusisahau kumshukuru Mungu kwa ajili ya wito wa kila mmoja wetu na
kwa ajili ya wawekwa wakfu wote, ambao bila kukoma, katika karne nyingi,
wanashuhudia upendo wa kipekee kwa ajili ya Kristo na Kanisa, na wanatolea
maisha yao ili kuwapelekea msaada wote wanaohitaji. Kati yao, hata katika
nyakati zetu, kuna mashahidi wengi, wanaoshuhudia upendo hadi kumwaga damu kwa
ajili ya Kristo na Neno lake.
…Tukiuangalia mfano wa Mt. Ursula, ambaye maisha yake yaligeuzwa na kutafakari
kwa mfululizo fumbo la Moyo Mtakatifu wa Yesu Mteswa, tunataka hata sisi
kumwiga, tukichukua nafasi ya chochote kinachotokea katika maisha ya kila siku,
ili tuweze kukigeuza kiwe zawadi ya upendo kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya
kila mtu tunayekutana naye.
Tujifunze kutoka kwake jinsi ya kuweza kusikiliza maneno ya Yesu “NAONA KIU”
ili sala yetu, mateso yetu, utulivu wa moyo na uaminifu wetu katika kutekeleza
majukumu tuliyokabidhiwa, ziweze kukidhi yale matarajio ambayo Mungu ameyaweka
juu ya kila mmoja wetu na juu ya Shirika letu lote.
Tufungue mioyo yetu na pia jumuiya zetu kwa mahitaji ya mazingira ambapo
tunaishi na kufanya kazi. Tuwe na ujasiri, kama Mwanzilishi wetu Mtakatifu, wa
kwenda katika pembe zote za dunia alipo binadamu, jambo ambalo Papa Francisco
analisisitiza sana kwa Kanisa zima. Wote tunapaswa kuwajibika kwa ajili ya kazi
kubwa ya uinjilishaji wa Kanisa la nyakati zetu. Tusisubiri wakati mzuri zaidi,
maandalizi ya kielimu au afya bora zaidi. Katiba yetu, katika n. 85 inasema
kwamba: “…kila mmoja wetu, yoyote iwe kazi anayofanya katika jumuiya,
anashirikishwa katika utume kwa njia ya maelekeo yake ya ndani. Kwa njia ya
maelekeo hayo, sala yake, matendo ama ugonjwa vinapata umaana wa kitume.”
Hata sisi tuwe na ile tamaa kubwa ambayo tangu mwanzo wa maisha ya kitawa,
lilikuwa wazo ambalo limeongoza maisha ya Mt. Ursula: ningejua kupenda tu …na
kuwapa wote Mungu! Tamaa hii imetekelezwa kikamilifu katika maisha yake, na
hayo yamehakikishwa na maneno ya watu wengi ambao walimfahamu na pia kwa sababu
Mama Kanisa aliamua kumtangaza Mtakatifu
Mwaka huu, uwe nafasi sio tu ya kumshukuru Mungu kwa Sherehe na maadhimisho
mbalimbali, lakini pia kufanya utafiti wa moyo binafsi na wa jumuiya. Tuwe na
ujasiri wa kujiweka mbele ya Mungu na mbele ya jumuiya katika ukweli ili
shukrani yetu kwa ajili ya zawadi ya Mt. Ursula, iwe yenye matunda mengi zaidi
kwa ajili yetu, kwa ajili ya Shirika na kwa ajili ya Kanisa zima.
Tufikiri pia juu ya zawadi za kiroho ambazo tungependa kumzawadia Mwanzilishi
wetu katika siku yake ya kuzaliwa…
Nawasalimia kwa upendo
M.Franciszka Sagun