njoo uone...
Ilikuwa siku kama nyingine wakati nilipokuwa na tamaa ya kukuuliza:
“Je, Bwana unaishi wapi?
“Njoo uone! wewe unanitafuta? Njoo kwangu na utaweza kuona mahali ninapoishi.”
“Utakutana nami katika ukimya, utaweza kuongea nami,
uso kwa uso kwa njia ya sala.”
“Nakusubiri, njoo! Nawe utaweza kutambua maana ya kweli ya maisha yako ambayo wewe unatamani kuyapata”.
Jumuiya ya masista Wa-ursula wa Mkiwa inakusubiri…
njoo uone !!!