Masista wa UrsulaESPANSIONE-descrizione in lingua italianawa Tanzania

 

JUMUIYA


 

Wasichana waliojiunga na shirika waliongezeka  mwaka baada ya mwaka kwa hiyo

·         Mwaka 1994 imefunguliwa jumuiya ya

·         Dodoma iliyojulikana kama  “nyumba ya matumaini”. Lengo la nyumba hii lilikuwa ni  kuwapokea na kuwalea watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki kwa sababu ya ugonjwa wa ukimwi.

·         Mwaka 1997 ilifunguliwa jumuiya ya

·         Issuna na katika jumuiya hii kilianzishwa “Chuo cha Veta.

·         Mwaka 2002 tulianzisha jumuiya ya

·         Sukamahela na lengo ni kuwasaidia wagonjwa wa ukoma.

·         Mwaka 2003 tulifungua jumuiya

·         Kihonda Morogoro,  kule masista walifanya kazi Parokiani  na pia walifundisha katika shule ya chekechea.

·         Mwaka 2005 zilifunguliwa jumuiya ya

·         Hosteli ya Itigi ili kuwapokea na kuwasaidia wasichana ya shule ya sekondari ya Itigi,

·         jumuiya ya Mweka Moshi ili kusimamia shule ya msingi ya Mt. Ursula huko Kibosho

·         pia jumuiya ya Diagwa ili  kuanzisha shule ya chekechea na kuwasaidia waseminari wadogo wa Jimbo la Singida.

·         Mwaka 2006 ilifunguliwa jumuiya ya

·         Singida Mjini kwa lengo la kuwapokea masista ambao wanahitaji kulala wakati wakiwa safarini. Pia kufundisha dini katika shule za msingi,

·         na jumuiya ya Leto kwa lengo la kusimamia kituo cha watoto yatima cha “Ngaleku  Centre.

·         Mwaka 2007 ilifunguliwa jumuiya ya

·         Kisawasawa katika jimbo la Mahenge ( sasa ni Jimbo la Ifakara) kwa lengo la kufanya kazi parokiani, kufundisha katika shule ya chekechea na kusimamia dispensary ya parokia,

·         Pia jumuiya ya Morogoro-Kola kwa lengo la kuwapokea masista ambao wanasoma katika shule mbalimbali na katika chuo kikuu na  kuwapokea wasichana wa Chuo kikuu.

·         Mwaka 2009 ilifunguliwa jumuiya ya Damaida kwa lengo la kuanzisha shule ya chekechea na kuanzia mwaka 2013 hata shule ya msingi

·         Mwaka 2010 ilifungwa jumuiya ya Kihonda Morogoro na badala yake ilifunguliwa jumuiya ya

·         Padre Pio – Morogoro kwa lengo la  kusimamia shule ya sekondari ya P. Pio,

·         Mwaka 2011 ilifunguliwa jumuiya ya

·         Kibaigwa ili kusimamia na kufundisha katika shule ya chekechea na shule ya ufundi. Jumuiya hii imefungwa desemba mwaka 2014.

Mungu ametusaidia na anaendelea kutusaidia katika utume wetu na kwa sababu hiyo tunamshukuru na tunamsifu yeye kila siku