Masista wa UrsulaESPANSIONE-descrizione in lingua italianawa Tanzania

 

"Pendekezo kwa ajili yako..." - sista Rita Fiorillo


Tumezaliwa ili Kupenda

Wajibu wetu mkubwa sana ni kupenda.

Kumpenda Yesu, kuupenda Moyo wake Mtukufu kwa nguvu zetu zote, ili maisha yetu yawe tendo la upendo lisilo na mwisho kwa ajili ya Yesu. Upendo huo uwakao ndani kama moto mkubwa, utawale mawazo yetu ili yaelekee, daima zaidi kwake Mungu Baba yetu.

Upendo kwake Yeye, uamshe ndani ya mioyo yetu imani isiyolegalega katika wema wa Mungu. Imani yenye uwezo wa kukupa ukweli na hivyo tukijiaminisha kwa undani zaidi, tunangojea yote toka kwa moyo wa Yesu.

Tusiwe na imani inayolegalega wala tusipoteze kamwe utulivu wa moyo ambao unapatikana kutoka katika upendo wa Baba yetu, kwani Yeye tu ndiye anayeongoza kila kitu kwa mapenzi yake matakatifu. Imani hii ya kweli, isiyotikisika, ni mojawapo ya majaribu makubwa ya upendo ambao tunaweza kuutoa kwa Yesu.

Yeye ameshinda ulimwengu. "Msiogope, enyi kundi dogo! kwa kuwa Baba yenu amependa kuwapeni ufalme wake.." Ufalme ambao ni sehemu yenu, na ambao ninyi mnapaswa kuutafuta na kuueneza...bila kuhangaika na kitu kingine chochote.

“ Najua ni nani ninayemtumainia..."

Upendo kwa Yesu msulibiwa ungepaswa kuwa kiini cha maisha yetu yote ya kiroho...

Yesu msulibiwa, kwa mateso na kifo chake, ametustahilia neema yuu ya neema: Ekaristi Takatifu. Chochote kile kilicho kizuri, kitukufu na kitakatifu katika maisha yapitayo ya kawaida, kimeshuka duniani, toka kwenye msalaba...Katika msalaba upo wokovu, tumaini, upendo, furaha, kila jema letu, kwa sababu juu msalabani Yesu ametukomboa, akitufungulia 3

 

milango ya mbingu. Kwa hiyo, watu wachache wanajipa sharti la kumpenda hasa Yesu msulibiwa ... kuteswa pamoja naye... kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu. Tumpende Yesu... tujifunze kutoka kwa Yesu msulibiwa jinsi ya kumpenda Mungu, na jinsi ya kuwapenda wanadamu wenzetu: jinsi ya kuwa wanyenyekevu, kuwa wazi, watii; jinsi ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine, jinsi ya kufanya kazi kwa ajili ya utukufu wa Mungu na kwa ukombozi wa ulimwengu... “ SITIO “ (Naona kiu) ni mlio wa uchungu, ni kilio kitokacho katika kinywa cha Bwana, ambaye anateseka juu ya msalaba. Yesu ana kiu, anatamani watu wenye uwezo wa kumpenda Yeye... uwake katika mioyo yetu daima moto wa upendo wa roho nyingine. Tusali kwa ajili ya Mapadri. Tusali ili Bwana atume wafanyakazi katika shamba lake. Tunapaswa kuwa sadaka ambayo kimya kimya na kwa mfululizo inawaka; katika kazi, katika sala, katika kuteseka na bila kikomo tuombe neema kwa ajili ya Mapadri. Kila msalaba utakuwa mwepesi zaidi; kila maumivu yatakuwa mepesi; kila sadaka itakuwa nzuri zaidi, ikimulikwa na wazo hili: Yesu pokea toleo hili ambalo linakulilia mbinguni: Bwana tupatie Mapadri wema na watakatifu katika kanisa lako.Ni kitu kitukufu kushirikiana ili kumwokoa mwanadamu. Lakini ni kitukufu zaidi kufanya kazi kwa ajili ya utakatifu wa Mapadri na kusali kwa ajili kuomba uongezekaji wa wito wa upadri.

"Mjifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni

mpole na mnyenyekevu wa moyo “

Turudie kila siku: Bwana utuf'anye wadogo...Wadogo katika maisha na katika vitendo, maana katika vitendo ndipo kwenye ukweli. Wadogo na wanyenyekevu, kwa kuwa pamoja na watu na kuwapeleka kwa Mungu...Awali ya yote, msichukiane na yeyote wala kwa sababu ya aina yoyote. Tuweke mbali wazo lolote la kudhulumu linalo 4

 

tutenga...vishawihi hivi ambavyo vinafanya tuachane na amani, amani ile muhimu ya furaha ya ndani. Tamaa ya makuu ni mwanzo wa kuanguka. Katika hiyo inatoka chuki na wivu ambavyo vinauwa maisha ya ndani.

Tufurahi kama wengine wanashinda. Tunyenyekeane wenyewe kwa wenyewe, tunyenyekee kwa moyo. Tusitafute kusifiwa na kutukuzwa na watu. Tusijidai kujiona wenye haki daima na kutaka kulazimisha hukumu yetu kwa wengine. Tujifunze kutoka katika Movo wa Yesu kuwa wapole na wanyenyekevu. Wakimya tunapoongea, wakimya tunapofanya kazi. Tujifunze kuwa wanyenyekevu, na Bwana atakuwa pamoja nasi. Atabariki kazi zetu na upendo mtakatifu utatuunganisha. Tuwe wakimya na wanyenyekevu, kwa sababu unyenyekevu ni msingi wa fadhila zole. Unyofu ni unyenyekevu, na unyenyekevu ni chemehemi ya neema, ya amani na ya utulivu.

“Pendaneni kama mimi

nilivyowapenda ninyi“

Yesu baada ya kuanzisha Ekaristi Takatifu, alisema kwa mitume wake: "Nawapeni amri mpya: pendaneni ninyi kwa ninyi, kama mimi nilivyowapenda ninyi....Mkipendana, watu wote watajua kwamba ninyi ni wanafunzi wangu". Tufikirie upendo wa Yesu kwetu na ishara zote za upendeleo ambao Yeye ametupa: wema usio na mwisho, sadaka hadi kifo cha msalaba; wema kwa mitume, kwa wenye dhambi, kwa watu wote... kwa watoto waliokuwa wakitafuta kubembelezwa naye, kwa watesaji na wauaji wake mwenyewe. Kwa wema mwingi alizungumza nao, alivumilia udhaifu wao, aliwasaidia, aliwaponyesha na kuwasamehe. Tujaribu kuwa wakunjufu kwa wote. Wema kwa tabasamu la upendo mdomoni. Tufurahi wakati tunapoweza kuwatumikia ndugu zetu. Tusiwahukumu wengine na kama haiwezekani 5

 

kurekebisha tendo, tuache kuihukumu nia yao, ambayo ni Mungu tu anaweza kuifahamu. Tujue kushukuru hata kwa mambo madogo madogo, na kuipokea misaada hata kama tunaiona haisaidii. Tujifunze kuishi daima kwa amani na wote. Tupendane... Yawe mbali nasi mafarakano na wivu, mambo ambayo ni adui mkubwa wa upendo. Uwe mbali nasi, ubinafsi, ambao unafanya mtu ajifikirie zaidi yeye mwenyewe, akiwasahau wengine....

“Ishini kama Yesu kwa furaha ya wengine”

Tuwafikirie kwanza wengine, ili wajisikie vizuri, na baadaye sisi wenyewe, ikiwezekana iwe vizuri sana kujisahau kabisa. Ishini kama Yesu, kwa furaha kwa wengine, tukijipiga moyo kwa wazo hili: kila kitu mtachomtendea mmojawapo wa ndugu zangu walio wadogo, mnanitendea mimi”. Tuwape furaha wengine. Ni vigumu kuieneza furaha kati yetu. Inatakiwa tu moyo uliojaa upendo, tabasamu mdomoni, upendo katika maneno, utayari hata kwenye huduma ndogo za upendo zilizoangazwa na furaha. Hatuwezi kufikiri kiasi gani cha furaha kinaletwa na tabasamu kunjufu, na neno moja jema...Utulivu ni kwa roho, kama vile ambavyo jua ni kwa ardhi. Inahitaji kwa kweli nguvu nyingi ya kuchagua kujishinda na kuwa, watulivu, makini, wanyofu, waangavu hata katika shida, taabu, kushindwa, upungufu wa afya na mateso.Lakini, watu watulivu wanaweza kueneza furaha duniani! Wanaweza kuwapelekea watu baraka nyingi na burudani nyingi moyoni mwao. Nafikiri kwamba mojawapo ya kitendo kikubwa cha upendo ni utulivu huu usiobadilika ambao unaeneza mwanga popote. Mtu mtulivu anapita kimya. Labda anafikiri kwamba hafanyi lolote jema, na hajui kwamba ameamsha tabasamu nyingi kwa utulivu wake; ametia moyoni mwa watu wengi faraja; hajui kwamba mara kwa mara 6

 

ameweza kuipasha moto mioyo iliyokuwa baridi na iliyo migumu. Hajui kwamba ameondoa ulegevu wa moyo na kukata tamaa na ameeneza furaha nyingi, yeye hafahamu, bali Mungu anafahamu na anajua... furaha yote aliyoieneza kando kando yake. Mtu anayetii mapenzi ya Mungu ni yule tu, anayetafuta furaha katika utimilifu wa kuyatimiza yenyewe, anashinda, hata kila kitu, hutunza ndani yake utulivu huu mtakatifu, furaha hii yenye mwangaza. Umekosa nini ili kuwa na furaha? Ukiwepo karibu na chemchem ya furaha: Yesu kwenye Tabernakulo na kwenye Komunio ya kila siku?...Furaha hii, haitegemeani na mambo ya nje, inapaswa kumulika kwa nje na kutia joto moyoni mwa wengine. Kumbuka tena: mtu mwenye utulivu ni mtume. Anaongea na Mungu, kwa sababu anawaelezea wanadamu, bila maneno, lakini kwa tabasamu, kwamba ni vizuri kumtumikia Bwana na kwamba utumishi huu unaleta furaha na amani ambazo ulimwengu hauwezi kuzitoa. Kwa hiyo daima tuwe watulivu, wapole na wenye furaha. Twendeni kwa imani kumwelekea Mungu, kumwelekea Yeye! Komunio yetu iwe kiini cha maisha yetu. Moyo wetu utabaki macho kwa Yesu hata kama mwili uko kazini. Wakati wa muhimu zaidi katika siku ni ule wakati wa Komunio, wakati ambao Mungu na Bwana wetu, anakuja kumiliki katika moyo wetu maskini. Moyo ujifungue kabisa kwa Bwana wetu, uwe huru kwa tamaa kubwa zote na wasi wasi... Vyote ndani mwetu viwe kimya, ili Bwana

aongee. Bwana aongoze, Bwana atawale. Yeye tu aishi ndani mwetu.

Ee Yesu, utupatie daima upendo mkubwa zaidi! Twendeni kwa Yesu kama watoto kwa mama, kama rafiki mchovu na mwenye njaa aendaye kwa rafiki yake ambapo anajua atapata faraja na msaada. Tumwambie Yeye chochote kile kilicho moyoni... Tusubiri na tujifungue moyo ili kupokea tumaini: Yesu mwenyewe anafanya kazi. Tusimkimbie. Shida zote na taabu zinaweza kutufanya nini? Haziwezi kutuondolea 7

 

Yesu. Na, wakati wote tunapokuwa na Yesu tunayo furaha ya mbingu, mwanga wa mbingu na mbingu yenyewe. Chochote kile cha duniani kitakuwa kidogo mbele ya ukweli huu! Tufungue wazi mioyo yetu ili kupokea upendo... na tutaweza kusema kwa hakika: " Yesu ananipenda ".Yesu ni hazina yetu. Tufike kwake, tufanye kazi kwa ajili yake aliye chemchem ya furaha yetu, ya amani yetu, ya raha yetu duniani, kwa wakati wote wa maisha na kwa milele.

Maskini pamoja na maskini

Twahudumia maskini na wadogo, hivyo hata sisi, katika maisha yetu yote tu wadogo na maskini! Tusitamani kuwa na nyumba nzuri na za kifahari... Tufuate ufukara huu: nyumba maskini... maisha bila vitu vya kifahari... chakula cha kawaida... tupende nguo rahisi. Tusitamani fadhili na tufurahi kama tutaweza kufanana na maisha ya jumuiya ya kawaida. Endapo mtu fulani atahitaji kitu zaidi ya kawaida, tuone kama kitubio na siyo kuking'ang'ania kwa moyo." Saf'i na maskini, siyo nzuri na ya fahari " uwe msemo wa watumishi maskini wa maskini. Tukiwa maskini katika maisha na katika kutamani, tutaweza kwa urahisi kuuelekeza moyo kwa Mungu. Na ikiwa mara kwa mara tunaumia kwa matokeo ya umaskini... tusilalamike.... Bali tufurahi, kwa kuweza kumuiga, angalau kidogo Yesu msalabani, ambaye hakuwa hata nguo. Kadiri tutakavyokuwa na vichache kwa ajili yetu, ndivyo tutakavyoweza kuwasaidia maskini zaidi. Tusione aibu kufanya kazi, kazi haimshushii hadhi mwanadamu. Tufanye kazi kwa ajili ya Mungu na tujitahidi kuwa tayari kwa kazi yoyote...Kazi zetu zinapaswa kuwasaidia maskini; ni kwa ajili yao Yesu alisema: “Kila kitu mtakachomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mtanitendea mimi.“ Napendelea kuwaoneni katika umaskini na kazi. Ninawashauri 8

 

kujinyima kwa kazi na umaskini wetu... kujinyima huko kusionekane na wengine....Maisha ya kitawa yanapaswa kuwa maisha ya kujinyima, kama sivyo sio maisha ya kitawa. Fanyeni mazoezi katika kujinyima kwa yale muhimu zaidi tunayokutana nayo kila siku. Tunahitaji kujinyima kwa kuishi katika amani na kwa umoja; kwa kuwa wakarimu na wakunjufu: tunahitaji kujinyima katika kusali kwa uelekevu; kwa kufanya kazi kwa uthabiti, kwa kutii kwa uaminifu na kwa ushujaa, kwa kuishi siku zote katika utulivu wa moyo. Hatuhitaji kuzitafuta nafasi hizi, zinajileta zenyewe ikiwa twajua kuzifaidi.

“Watii katika imani ”

Kama utii unatokana na imani, itakuwa rahisi zaidi kwetu kuyatimiza mapenzi ya Mungu.

Tukipenda mapenzi ya Mungu tutapenda utii unaotupa, kwa hakika, nafasi ya kuyatimiza kwa mfululizo mapenzi ya Mungu.Tupende utii, ambao unaweza kubadilisha maisha yetu yote kuwa dhabihu ya upendo safi kwa ajill ya Mungu. Tusijiunge na kundi la wale wanaopenda utii ikiwa unalingana na matakwa yao wenyewe, lakini hukimbia mbali au hunung'unika wakati utii hauwapendezi wao. Katika kila kitu na katika kila nafasi tujibu daima“ Tazama, mimi ni mtumishi wa Bwana: Kama Mungu anavyopenda“. Tusikilize, tutii kwenve mambo madogo. Tusikilize, tutii kwenye mambo makubwa. Tusikilize daima...Tunapokuwa wazee zaidi, lazima tuwe wenye utii zaidi. 9

 

“Salini bila kuchoka”

Maisha ya sala yanapaswa kuwa daraja linalounganisha wakati wa sasa na wa mliele, mbingu na dunia, mwanadamu na Mungu. Bila sala, hakuna maisha ya kiroho, hakuna kazi ya Mungu. Tusali ... bila kuangalia kwamba tunapata kitulizo au ukavu wa moyo... tusali kwa utukufu wa Mungu. Yesu anasema kwamba inapasa kusali daima, bila kuchoka. Tutafute wakati wole umoja na Mungu... Katika kazi tuelekeze mawazo yetu kwa Mungu, kama maua yanavyoelekea jua. Tazama furaha ya roho: kukaa ndani ya Mungu na pamoja na Mungu. Kama ni hivyo hata katika mahangaiko, mateso, umaskini wa maisha, mionzi ya nibingu, ya amani, ya imani, ya furaha, itawaka daima kwa ajili yetu. Katika sala hii ya mfululizo tunapaswa kufanya mazoezi bila kukata tamaa...

Tusali, tusali kwa imani. Kabla ya kuanza sala tufanye nia thabiti kwa imani ya kweli, ya ndani. Je, unataka kuishi kabisa pamoja na Bwana?... Uyatimize kwa ukamilifu Mapenzi Yake....

Sala, kitubio, upendo: tazama kwa jumla maisha yetu. Sala nzuri kuliko zote? Kuyapokea Mapenzi ya Mungu. Upendo mzuri kuliko wote? Kuyatimiza kwa imani Mapenzi ya Mungu. “ Kama Mungu apendavyo, kama Mungu apendavyo ". Kwa maneno haya mdomoni tutayapita maisha, katika dhoruba kwa utulivu, wenye nguvu katika vita, wenye upendo katika chuki, watakatifu katikati ya wakosefu .... " Kama Mungu apendavyo ". Ili kuwa na umoja kabisa na Mapenzi ya Mungu, tunapaswa kuyatimiza siyo kwa uaminifu tu, bali hata kukubaliana nayo kwa kupokea kila kitu Mungu anachotaka kuamua juu yetu. Tuweze kuwa na uhakika wa kweli kwamba kila kitu Mungu anachotupatia ni kwa ajili ya wema wetu. Kwa hiyo tubaki watulivu katika Mapenzi ya Mungu, tukishindana dhidi ya wasiwasi, mahangaiko, woga unaoingia katika maisha yetu, mbele ya taabu na katika mateso ya ghafla. Je, kwa nini 10

 

tunafadhaika? Je, kwa nini tunahangaika? Itakuwa kama Mungu anavyotaka na itakuwa vizuri. “Kama Mungu apendavyo.” Maneno haya yaliyosemwa kwa upendo, yenyewe ni kitulizo kwa roho iliyo na uchungu. Kadiri zaidi itakavyoingia akilini mwetu kumbukumbu kwamba Mungu anatuangalia, kwamba sisi tuko mbele Yake, sala zetu zitakuwa rahisi na nzuri zaidi. Salini kwa imani, isiyo na mwisho, na kwa uthabiti. Mungu anatupatia hicho tumwombacho... lakini tunapaswa kusali bila kuchoka, hata kwa miaka mingi, tukiwa na hakika kwamba, Baba Mwema... anatupatia hicho tumwombacho kwa jina la Yesu Kristu. Tungekuwa na imani kubwa tungeweza kuihamisha milima. Tumpende Mungu, Baba Mwema sana. Tumpende Msulubiwa, Mwokozi wetu, tumpende Roho Mtakatifu ambaye anatutakatifuza na Mama Yetu Mbarikiwa Maria. Kadiri tunavyosikia kidogo moto wa upendo, hivyo hivyo tutafute kwa uthabiti, katika ukavu wa moyo, kumwonyesha Mungu upendo wetu. Tusali kwa mfululizo, kama Yesu alivyotuamuru, kwa sadaka ya matendo yetu yote kwa Mungu. Tupate faida ya kila muda ulio wazi...Tusali... sijui kuwashauri chochote kilicho nafuu zaidi: maisha yetu yote duniani yawe sala, na Bwana atakuwa pamoja nasi. Katika sala tutampata Yeye ambaye anatupenda. Katika sala tutabaki pamoja Naye na tusimwachilie kamwe.

“ Mimi nitakupeleka nyikani na kusema nawe

maneno ya kutuliza moyo “

Ukimya ni amani ya roho. Kwenye ukimya uweke katika Moyo wa Yesu na Maria, masikitiko yako, matumaini yako na mahangaiko yako, umwombe na umshukuru. Furahi na vuta kwa moyo wazi, hewa ya milele iliyokuzunguka. Zoea kuelekeza moyo kwa Mungu... itakuwa tunda la jitihada kubwa. Asubuhi kusudia kumkumbuka Mungu siku nzima. 11

 

Wakati wa mchana jiulize kama umetimiza ulivyokusudia. Omba zawadi ya umoja huo. Pole pole bila wewe kutambua, utakuwa umeunganika kabisa na Mungu daima na Yesu atakuwa kiini cha maisha yako.

Epuka maneno ya bure na uchunguzi wa bure na... utaifikia mbingu hiyo duniani. Ni vizuri kuacha kufuata ushauri wako kwa ajili ya kufuata ushauri wa wengine, hata kama siyo mzuri sana, ili tusiharibu upendo wa kindugu. Tunapenda kazi ya kitume ienee? Tuishi kwa upendo na umoja.

Tunapenda kuzivuta roho kwa Mungu? Tuishi kwa upendo na amani. Kitu kinachodhibitishwa na mioyo ya wanadamu kwa jumuiya ya watawa, ni kuwa watu wanaoishi maisha ya umoja na upendo wa kindugu.

“Muwe watakatifu “

Ningependa kuwaombeni kwa mfululizo: “muwe watakatifu”. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu: kujitakatifuza kwenu. Muwe watakatifu na baraka ya Mungu itashuka katika jumuiya. Muwe watakatifu na kwa urahisi mtazivuta roho kwa Mungu. Tafuteni daima na kabla ya yote ufalme wa Mungu na haki yake. Na, tena nawaomba: ishini katika amani na kwa umoja, katika ukunjufu wa upendo kwa kufanya kama wakristu wa kwanza, " moyo mmoja na roho moja ".

Pale panapokosekana amani na umoja, haiwezi kuwepo baraka ya Mungu wala utakatifu. Muwe wanyenyekevu na mtajua kuutunza upendo huu mtakatifu, umoja huu na imani hii. 12

 

“ Tazama Mama yako …“

Tumpende Maria. Mapenzi ya mwisho ya Yesu msalabani ni kwamba sisi tuwe watoto wa Maria...Tumkimbilie Yeye, kwa imani kubwa. Tusiruhusu kamwe ulegevu wa moyo uingize mioyoni mwetu ukosefu wa matumaini. Tuwe na uhakika kwamba Maria anatupatia msaada kwa mwujiza kuliko kutuacha. Tupende kile kimpendezacho Maria. Tupende Rozari.Yawe haswa ya thamani maneno ya Bikira Maria yaundayo tamko rasmi la Shirika letu:" Tazama mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema ".Tuwe kama Yeye watakatifu ... watumishi waaminifu wa Mungu. Daima tuwe tayari kuyatimiza mapenzi yake; mapenzi yakiwa wazi na ya kupendeza au yakileta misalaba na uchungu. Kama Maria alisalimu kila aina ya mapenzi ya Mungu kwa maneno yaliyosemwa naye siku moja na yaliyotendwa katika maisha yake yote, hivi hata sisi kwa mfano wake, tuwe daima wakimya watumishi wa Bwana, wanaoyapokea mapenzi yake yoyote kwa tabasamu mdomoni na kwa " FIAT " ( iwe kama utakavyo wewe ) na " DEO GRATIAS “ ( kumshukuru Mungu) moyoni, hata kama kuna machozi machoni. Tumpende Maria, tupende Rozari na, niaminini ninaposema: upendo bora zaidi kwake ni ule wa kuwa, kwa mfano wake, wakimya, waaminifu, wanyenyekevu, watumishi wa Bwana wanaorudia kwa mfululizo kwa moyo na kwa matendo: Tazama, nitendewe kama Mungu apendavyo, kama Mungu apendavyo!

“Mvumilie kwa imani“

Yesu anasema: "Atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa ". Tazama jambo muhimu zaidi: kuvumilia.

Kumbuka kwamba maisha yote ni mashindano, hatuwezi kusema kwamba haina maana kushindana, kwa sababu 13

 

kupigana na kuvumilia katika shida, ndicho kinachomfurahisha Mungu. Isingekuwa vigumu kuwa watakatifu kama kila juhudi ya kudumu kidogo, ingekuwa faida ya kutupatia ushindi

halisi. Mara kwa mara, Bwana anapenda uvumilivu huu ambao mbele ya ushindani mkubwa, haurudi nyuma, ambao kila siku huanza tena, na kwa utulivu na kwa imani, husubiri hadi Mungu aufanye wenye ushindi. Naamini kwamba Mungu mara nyingi anafurahi zaidi kutuona tunavumilia kuliko kutuona tunashinda kwa urahisi na kwa muda tu. Kwa hiyo muwe wavumilivu. Wavumilivu katika nia na katika maazimio. Wavumilivuu katika sala na katika mazoezi ya fadhila na sadaka ndogo. Mara kwa mara, tukiona kushindwa, tukiona kwamba hatuendelei mbele, tunakata tamaa. na tunaacha kila kitu: " nimeshindwa, hiyo haina maana". Lakini inafaa kujikaza, inafaa! Kadiri ulakavyoomba kwa muda mrefu zaidi, utapata kwa kiasi kikubwa zaidi. Mara nyingi tunaacha kuomba zawadi za kiroho kwa sababu tunazo shuguli za dunia zinazotupendeza zaidi. Tungeomba kwa uthabiti daima kitu kimoja , ni kweli Bwana angetulipa sala zetu. Sisi tukikosa uvumilivu huu hatupewi kitu tunachopaswa kupewa, kwa sababu ukosefu wa uthabiti katika tamaa, unatufanya tusijue kitu tunachoomba kwa kweli. Mvumilie... msifanye ukosefu wa matumaini uwashike ninyi. Haidhuru kama tutaanguka hata mara mia moja,, ikiwa tutainuka mara mia moja na kuendelea na safari kwa imani na juhudi. Kila siku tuanze mwanzo; tusifikiri kwamba ni muhimu kuona maendeleo yetu. Inatosha tukiwa na nia njema. Nia hii ikitusukuma, tunaweza kuendelea mbele kwa imani na uthabiti.