UTUME
Tangu mwanzo wa Shirika la
“Waursula” lililoanzishwa na Mtakatifu Anjela Merici, waursula wote duniani ni
walezi na walimu wa watoto na vijana.
Waursula kadiri ya karama yao wanafanya utume wa katekesi, kazi za Parokiani,
vyama vya kitume, utume katika shule mbalimbali kama walimu wa shule za
chekechea, wa shule za msingi,
za ufundi
na sekondari,
ziwe za serikali au za binafsi.
Tanzania utume wa masista unaelekea zaidi katika kutoa elimu ya kiroho na maadili kwa njia ya vyama vya kitume katika Parokia, kwa njia ya kufundisha katekesi, maandalizi ya sakramenti na mara kwa mara kuwandaa watu wazima na wazee kuwa wakatekumeni.
Masista wanafanya kazi kwa watoto na vijana katika nyumba za watoto yatima na katika Hosteli zinazopokea wanafunzi wa shule za sekondari, za ufundi na hata wanafunzi wa Vyuo Vikuu.
Katika nyumba ya watoto yatima – Dodoma – masista wanachukua nafasi ya wazazi (kama mama) wa watoto hayo yatima ambao wazazi wao wamefariki kwa sababu ya ugonjwa wa ukimwi.
Na katika nyumba ya Leto-Rombo masista wanachukua nafasi ya mama wa wale watoto wachanga wakiwapa watoto wa miezi michache ule upendo ambao wameukosa kwa sababu mama zao wamefariki au wamewatupa.
Wapo masista wachache ambao wanafanya kazi ya unesi na ukunga hasa katika zahanati. Wapo masista ambao wanafanya kazi katika Hospitali ya Mt. Gaspari-Itigi, mmoja kama daktari ya watoto na mmoja kama nesi-mkunga.
Katika kijiji cha Sukamahela masista wanatoa huduma kwa wakoma na Mkiwa masista wanawahudumia pia wazee walioachwa peke yao na ambao wanahitaji chakula, nguo na hata nyumba.
|
||