Masista wa UrsulaESPANSIONE-descrizione in lingua italianawa Tanzania

 

Maneno machache ya Mtakatifu Ursula


 

 

Nendeni duniani kote
mkiwa na tabasamu mdomoni mwenu.
Nendeni mkasie mbegu ya furaha,
mtabasamu na wote,
hasa kwa wenye huzuni moyoni,
waliokata tamaa na wanaokandamizwa…
Mtabasamu kwa tabasamu ile
itakayowaeleza  watu
wema wa Mungu

 

“Watakatifu hulelewa magotini mwa mama
yao mwenyewe, ambaye ni mtakatifu”

“Niko mikononi mwa Mungu na
sijaacha kurudia mara kwa mara:
Kama Mungu apendavyo”

 

“Ee Bikira Maria , utufundishe kuwa daima
watumishi wakimya wa Bwana, ambao
wanatamani kitu kimoja tu: mapenzi ya
Mungu yatimizwe na siyo mapenzi yetu”

“Tunafanya kazi kwa kutegemea
uwezo wetu, ujuzi wetu, akili yetu,
lakini kidogo tunamtegemea Mungu”

“Nenda kazini pamojana Yesu,
fanya kazi mbele ya macho yake;
fanya kazi kama Yeye alivyofanya zamani,
kwa jasho la uso, na kazi yako itageuka kuwa
sala safi kabisa.”

“Sala iliyo bora kuliko zote
ni kujiweka daima katika mapenzi ya Mungu,
kitubio kikubwa zaidi ni kukubali
kimya kimya kuyatimiza mapenzi ya Mungu,
upendo ulio mkubwa zaidi ni kutimiza kwa
uaminifu mapenzi ya Mungu“

“Ishini kama Yesu
kwa ajili ya furaha ya wengine”

Litokee lile litokealo: ninyi bakini katika
ukweli wa heri ambao Moyo wa Yesu
atawaongoza kwa njia njema hata kama
imeoteshwa miiba. Iweni na imani, wanangu,
kuweni na imani, hata kama upeo
wa maisha ungekuwa mweusi kama usiku.

“Maisha ya sala ni daraja
linalounganisha wakati wa sasa
na wa milele, mbingu na dunia,
mwanadamu na Mungu”

“Hakuna upendo bila sadaka”

“ Mtu mwenye furaha, ni mtume ambaye,
bila kufahamu anawapeleka wengine kwa
Mungu”

“Tabasamu lililo juu ya uso mtulivu
linazungumzia furaha ya ile roho ambayo ina
umoja na Mungu, linazungumzia amani ya
dhamiri safi, ya kujitupa pasipo mawazo
mikononi mwa Baba wa mbinguni.”