WOSIA


 

MANENO YANGU YA MWISHO KWA WATOTO WANGU WAPENZI

         

MANENO YANGU YA MWISHO KWA

WATOTO WANGU WAPENZI

Wanangu wapendwa kazi hii ambayo ni maagizo yangu kwenu imekwisha. Ningependa kuwaombeni bila kuchoka wanangu: tafuteni nafasi ya kwanza ambayo ni utakatifu. Hilo ndilo kusudi ambalo mmelijia mlipoingia Shirikani, haya ndio mapenzi ya Mungu: kujitakatifuza kwenu. Iweni watakatifu, na baraka ya Mungu itabaki katika Shirika letu.

Iweni watakatifu na kwa urahisi mtawavuta wengine kwa Mungu. Iweni watakatifu na furaha tukufu itabaki kwenu. Iweni watakatifu na mtakuwa watulizaji wa Moyo wa Yesu katika mateso. Iweni watakatifu!

Ni furaha kiasi gani nitakayoipata nitakapoangalia toka mbinguni watoto wangu ambao hujitahidi kuishi kwa bidii katika njia ya usahihi. Tafuteni awali ya yote ufalme wa Mungu na haki yake (Mt.6,33).

Kwa mara nyingine tena nawaomba, wanangu, ishini kwa umoja, kwa kupatana na kwa upendo wa moyo, uliolindwa kama Wakristo wa kwanza, "Moyo mmoja na roho moja" (At. 4,32). Pale panapokosekana umoja na uelewano, hamwezi kupata baraka ya Mungu wala utakatifu.

Iweni wanyenyekevu, na mtafahamu kuutunza huo upendo mtakatifu, huu uelewano na umoja katika Mungu. Ni afadhali hukumu yenu, hata kama ni nzuri, ishindwe, kutokana na matokeo ya kutokuwa na wema kama wengine, kuliko upendo wa kindugu uharibike.

Mnapenda kazi iongezeke? Ishini katika upendo na uelewano.

Mnapenda kuwa watakatifu? Ishini katika upendo na uelewano.

Mnapenda kuwawuta wengine kwa Mungu? Ishini katika upendo na uelewano. Hakuna chochote kinachoweza kusemwa 56

kwa moyo wa kibinadamu kwa ajili ya Shirika la watawa lililounganika kwa kifungo cha uelewano na upendo wa kindugu.

Jaribuni hivyo kwamba, masista wajisikie vizuri kuwa pamoja nanyi. Saidieni mawazo yao kwa yale yawatiayo huruma kwa wajibu wenu. Wekeni mbele furaha yao na yenu, na Mungu kwa baraka yake atakuwa pamoja nanyi. Naamini kwamba nitalia mbinguni, kama nitawaona wanangu waliotengana, ya kwamba wanashindana na hawapatani kati yao. Ni afadhali kwamba Shirika letu liache kuendelea kuliko itokee utengano na kutosikilizana. Mungu awaepusheni!

Na sasa nawaaga tena kwa mara nyingine watoto wangu. Nawaomba kama mnanipenda, onyesheni upendo, heshima na utii kwa yeye atakayenipokea, kama kifo kitanikuta katika cheo cha Mkuu wa Shirika. Msiyafanye magumu, maisha ya mkubwa wenu, rahisisheni daima, daima nawaomba kwa moyo wote.

Mungu awe nanyi! Salini kwa roho yangu maskini yenye dhambi. Msimsahau Mzee Mama yenu ambaye atawapenda daima na daima atasali kwa ajili yenu, na daima atawabariki watoto wake: Kwa Jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu. Amina.

Pniewy, Sant'Olaf, 28.10.1924