WOSIA
VI.
AGIZO LA SITA
SALA
Hatupaswi kuishi kwa ajili ya dunia bali kwa ajili ya mbingu. Na kwa mbingu ni kuishi kwa kujiunga na Mungu kwa sala. Sala kwa kweli ni daraja linalounganisha wakati na umilele, dunia na mbingu, mwanadamu na Mungu. Kwa hiyo maisha ya mtawa yanapaswa kuwa maisha ya sala.
Nafasi ya kwanza ni kufuata kwa uhakika na usawa mazoezi ya kiroho inavyoelezwa kwenye Katiba yetu. Inapowezekana, msiache bila sababu maalum. Huu ndio kweli, wajibu wenu kwa Aliye Juu. Mungu awasaidie msiziache, kwanza mzifuate kwa dhamiri kubwa ya juu kabisa.
Mwenye upendo wa kweli, anafanya, anajaribu, na kwa kawaida, anapata muda wa wajibu huu muhimu ambao ni mazoezi yetu ya kiroho. Haya mazoezi yatakuwa ndio kuzivutia kwenu neema, mwanga, msaada wa Mungu, yatakuwa ndio kuwashushia kwa maisha yenu yote baraka zake. Bila sala hakuna maisha kwa Mungu hakuna huduma kwa Mungu! Watoto wangu, fuateni kwa uaminifu mkubwa mazoezi ya kiroho bila kuangalia kwamba mnapata kitulizo au ugumu. Sio kwa kujitosheleza kwenu, bali kwa ajili ya utukufu wa Mungu muwe waaminifu katika hilo, mkipigana kwa ushujaa dhidi ya ulegevu, uvivu unaofanyika kwa kujifanya kwa njia mbali mbali, ili kujitoa katika sala. Salini kwa imani na kwa juhudi siku kwa siku!
Sista ambaye ni mwaminifu katika ukimya, asiyefanya uchunguzi wala kujiingiza katika mambo ya wengine, anapata muda wa kutimiza wajibu wake wa kiroho. Inawezekana wakati mwingine kutokea hivyo, kwa hiyo, wanangu, ombeni daima ruhusa. Na, kama hamna muda wa kuomba, mnapaswa baadaye
21kumweleza mkubwa wenu. Msizoee kujiruhusu wenyewe.
Kristo alisema kwamba tunapaswa kusali daima, bila kuchoka (Rejea, .Lk.18:1). Msijiwekee mipaka kwa mazoezi ya kiroho tuliyoombwa kwenye Katiba yetu. Hapana, hiyo ni kidogo mno kwa roho! Tafuteni muungano wa daima na Mungu kwa njia ya nia zenu, mnazozifanya mara kwa mara, kwa mfululizo wa sala fupi (za mishale), zikiongoza mawazo yenu, hata wakati mkiwa kazini, kwa Mungu, kwa Yesu wenu, kama ua linalo elekea jua.
Haya ni furaha ya roho: kuwa katika Mungu na pamoja na Mungu. Hivyo, chochote kile cha kidunia kionekanacho kidogo hivi, na pia katika shida, mahangaiko, maafa, umaskini na mateso ya maisha panawaka daima mionzi ya amani, ya matumaini na furaha.
Katika mwendelezo huu wa sala mnapaswa kufanya mazoezi bila kukata tamaa, pale ambapo hakuna matokeo ya yale mliyoomba. Inahitaji kujaribu, kujaribu tena na kujiimarisha na kazi hiyo - kama imefanywa kwa upendo - itampendeza Mungu, hata kama inaonekana haina matunda.
Salini daima kwa imani. Hilo ndilo shauri langu, watoto wapendwa; msifikiri mnapoteza muda. Mwanzoni mwa kila sala wekeni nia thabiti na imani ya kweli ya ndani. Kadiri zaidi itakavyoingia akilini mwetu kwamba Mungu anatuona, tuko naye, tunasali chini ya miguu yake na kwamba tunajishikilia kwenye Moyo wake Mtukufu, ndivyo zaidi sala itakuwa rahisi na itapokelewa.
Salini kwa imani bila kikomo na kwa uvumilivu.
Mungu atatupa kwa uhakika hicho tumwombacho, kama kinaleta manufaa mema ya kiroho, lakini tunapaswa kusali bila kuchoka, hata kama ikiwa ni kwa miaka mingi, kwa uhakika wa moyoni, kwamba Baba mwema wa mbinguni atatupatia hicho tunachomwomba kwa jina la Bwana Wetu Yesu Kristo. Kama
22