WOSIA
V.
AGIZO LA TANO
UTII
Kama unyenyekevu ulivyo mzizi wa kila wema, hivi hivi utii ndivyo ulivyo msingi wa kila fadhila za kitawa. Kama mnapenda kuwa watawa wema na watakatifu, hamna budi kuotesha ndani mwenu utii kamili. Utii unapaswa kujengwa juu ya imani, bila hivyo hautakuwa kamwe utii kamili. Mnapaswa kuamini kabisa kwamba kwa kupitia mkubwa wenu Mungu anaongoza nyumba zetu; kwamba Mungu kwa njia wa wakubwa wenu, anawapeleka, anawaongoza njia ya kufuata, anawafunulia mapenzi yake. Uamuzi wa viongozi ni Mapenzi ya Mungu kwa masista. Kwa hiyo, kumsifu Mungu ni pamoja na kuwaheshimu, kuwapenda na kuwatii wakubwa wenu.
Katika nyumba zetu zote, iwe nyumba mama au nyumba ya Senta au katika jumuiya ndogo, Mama mkubwa au kiongozi awe amezungukwa na heshima kubwa na upendo, na hayo yote ni kwa ajili ya Mungu. Wanangu, mmemzunguka kwa heshima kubwa Mama yenu mzee, na mimi daima nimepokea ishara hizo nikielewa kwamba, chochote kile chema mlichonifanyia, mmefanya pia kwa Mungu, na kwa Mungu hakuna chochote kilichozidi. Hicho mlichokifanya kwa Mungu katika nafsi ya Mama yenu mzee, wapeni pia kila mkubwa au kiongozi kwa sababu katika wao mnamsifu Mungu, ambaye anastahili kuheshimiwa, kama mlivyofanya, kwa Mama yenu mzee, na kwa kiongozi yeyote aliye kijana au mzee. Shirika letu, ambalo msingi wa wema wake ni unyenyekevu, linapaswa kujitofautisha kwa heshima na staha wanazopewa wakubwa.
Msidhani kwamba, umri unatuzuia sisi kutumia alama za heshima zilizokuwa katika desturi yetu, kwa mfano: kupiga magoti mbele ya mkubwa. Kupiga magoti haipo tena kwenye
18desturi, wakati unapoomba kitu fulani, wakati yeye anapotuonya, wakati wa kuomba msamaha au baraka; au kuinuka wakati mkubwa anapoingia darasani, mezani au kwenye vyumba vingine nk.; au kuomba msamaha na kushukuru mezani, nk. Hata ikiwa katika umri mkubwa wa sista, hata umri wa kijana wa mama mkubwa au kiongozi hiyo haituzuii. Mungu yule yule yuko kwa wazee na pia kwa vijana wakubwa wetu. Na sisi wazee na vijana tuko daima "wadudu wadogo" mbele za Bwana ambapo kwanza tunapaswa kusujudia kwa unyenyekewu mkubwa. Kwanza, walio wazee zaidi waoneshe mfano mzuri kwa walio vijana, wakiwafundisha kwa matendo namna wanavyopaswa kuwapa heshima wakubwa wao, kwani katika wao twamsifu Mungu.
Viongozi ambao ni vijana watambue kuwa hizi alama za heshima katika desturi za Shirika letu, zinatolewa kwa Mungu, katika utu wao, na waelewe kuwa siyo haki yao kwa unyenyekevu wa uongo na kusamehe masista bila maana, sababu zile alama za heshima na upendo hazitolewi kwao, bali kwa ‘Aliye Juu’
Nawaomba tena kitu kimoja, watoto wangu wapendwa: sikilizeni kwa heshima, kwa unyofu na upendo, mikutano ya wakubwa. Hakuna atakayefikiri kwamba hahitaji, sista asifikirie kwamba anafahamu zaidi ya wao jinsi ya kutenda na kuishi. Msiondoe desturi ya kutayarisha kila jioni tafakari ya moyo ya siku inayofuata, kwa kusingizia kuwa mawazo ya mkubwa hamkubaliani nayo. Hapana, wanangu, hapana! Kutenda hivi, ni ishara ya kiburi. Kumbukeni kwamba Mungu anaongea nanyi kupitia kwa wakubwa. Sikiliza kwa unyenyekevu , uelewe na kukubali kwamba unahitaji mafundisho ya Mama Mkubwa. Na hata kama mara kumi hujapata kitu chochote kinachofaa katika vipindi vyake, inawezekana katika safari ya kumi na moja Bwana atatumia maneno ya mkubwa ili kuufumbulia
19moyo wako hazina za Moyo Wake Mtukufu, zile hazina ambazo, wewe peke yako labda kamwe usingezigundua .
Kama utii wenu unatokana na imani, haitawawia vigumu kuyatimiza mapenzi ya Mungu yaliyoelezwa kwenye Katiba, kwenye Desturi na kwenye mapenzi ya Viongozi. Kama mnapenda mapenzi ya Mungu, mtapenda utii ambao utawapa uwezo wa kutimiza kila wakati mapenzi ya Mungu. Ni furaha gani inayotokana na wazo hilo:"Siku nzima, kuanzia asubuhi hadi usiku, na - kuanzia usiku hadi asubuhi, nafahamu wazi mapenzi ya Mungu kwangu, na kwa hayo mapenzi naweza kuendelea kudumu katika ushirika huo"
Pendeni utii, ambao utayageuza maisha yenu yote kuwa kama sadaka ya upendo safi kwa Mungu. Msipende kujiunga kwenye idadi ya zile roho zinazopenda utii wakati tu pale mapenzi ya wakubwa yanapatana na yao wenyewe, lakini hata wanachukia na kunung'unika wakati mapenzi ya wakubwa sio wapendavyo wao. Hapana, hapana! Tiini daima, hata japokuwa mapenzi ya wenye madaraka yanawapendeza au hayawapendezi; katika mapenzi yao mtakutana na mapenzi ya Mungu, na hiyo inawatosha. Kuweni tayari kwa kila ishara za mapenzi ya wakubwa wenu na katika kila amri jibuni daima: "Mimi hapa ni mtumishi wa Bwana" (Lk.1:38). Kama Mungu apendavyo! Pendeni ule utii mtakatifu! Wanangu wapendwa wasifuni, waheshimuni na kuwatii wakubwa wenu na Mungu atakuwa pamoja nanyi. Nawaombeni kwa unyenyekevu, timizeni agizo hili la Mama yenu mzee, sababu hata katika lenyewe ni kweli kwenu ni mapenzi ya Bwana. Tiini kwenye mambo madogo, tiini kwenye mambo makubwa, tiini daima na popote. Mnapokuwa wazee zaidi, hivyo zaidi muwe watii: Tiini!