WOSIA


IV.

AGIZO LA NNE

UMASKINI

 

        

Kumbukeni, watoto wangu, kwamba umaskini ni ukuta mkuu wa roho za kitawa na kwa hiyo mnapaswa kuupenda kwa moyo wote.

Shirika letu linapaswa kuwahudumia wadogo na maskini na kwa hiyo hata sisi, katika maisha yetu yote tunapaswa kuwa wadogo na maskini. Msitamani kuwa na nyumba nzuri, kubwa, zenye fahari, za kujifurahisha. Hapana, hapana! Nawasihi, watoto wangu kwamba kama wakati wa maisha yangu nyumba zetu zilikuwa maskini sana, maisha yetu mara si ya kuridhisha, na chakula cha kirahisi sana, hivi hata baadaye shikeni hicho kilichoandikwa kwenye kanuni zetu. Tamaa zenu ziwe daima zikielekea umaskini. Pendeni vazi lenu la kimaskini, na msione aibu kama wakati mwingine litakuwa na kiraka, ilimradi tu liwe safi.

Msitamani jambo la zaidi ya kawaida, furahini kama mnaweza kugawana kwa wote hicho kinachopatikana katika jumuiya. Na kama mtu fulani anahitaji kitu zaidi ya kawaida, aone ni kama kitubio na sio kukishikilia kwa moyo. "Safi na maskini", siyo "nzuri na ya fahari, ya kujifurahisha" uwe ni msemo toka kwa maskini mtumishi wa maskini.

Mkiwa tu maskini katika maisha, maskini katika kutamani, itawawieni rahisi kuielekeza mioyo yenu kwa Mungu, ambaye ni hazina pekee ya moyo mkamilifu katika umaskini. Na kama wakati mwingine mnapaswa kuusikia ugumu wa umaskini, kwa mfano wamesahau kuwapa hicho mlichoomba, au mkifanya majaribio ya ukosefu wa kitu au mkipata kitu kibaya zaidi ya wengine, msilalamike na msijiachie kuchukuliwa na maelekeo mabaya, msijiachie 15

kutawaliwa na wivu. Furahini haswa kwa kuweza kumfuata, angalau kidogo, Yesu Msalabani, maskini, aliyevuliwa hadi nguo.

Zaidi tukiwa maskini, ndipo zaidi twaweza kuelewa maneno ya Mt. Fransis, maskini wa Assisi: "Mungu wangu na yote yangu". Kadiri tutakavyohitaji vichache kwa ajili yetu wenyewe, ndivyo zaidi tutakavyoweza kutoa kwa maskini.

Umaskini umeunganishwa sana na kazi. Tuko maskini na kwa hiyo, tunao wajibu wa kupata chakula kwa ajili yetu wenyewe na kwa ajili ya watoto wetu maskini. Kazi, kazi ngumu ya maskini ndio wajibu wetu. Kama maskini anavyofanya kazi kwa jasho lake usoni, hata kama mifupa inamuuma na anasumbuliwa na usingizi, sababu anajua anapaswa kufanya kazi, la sivyo yeye na watoto wake watabaki bila chakula, vivyo hivyo hata sisi tunapaswa kufanya kazi. Hatukuja hapa konventini ili tuchoke kidogo zaidi ya walimwengu, bali tumekuja ili tufanye kazi zaidi na ngumu zaidi. Katika ulimwengu tunafanya kazi kwa ajili yetu, badala yake hapa shirikani tunafanya kazi hasa kwa ajili ya Mungu ambaye amekuja na amefanya kazi kubwa kwa ajili yetu na ametoa uhai wake kwa ajili yetu.

Tusione aibu ya kufanya kazi. Hakuna kazi inayomdhalilisha mwanadamu. Nenda kwenye kazi ile uliyopewa kwa utii bila kujiuliza ni ya maana zaidi au hapana, ya kunyenyekesha, au ya juu na ya heshima. Fanya kazi kwa ajili ya Mungu tu, na uwe daima, daima tayari kwa kazi yoyote ile. Mungu aepushe hasira kati yenu kwa sababu ya kazi aliyopewa mtu kuwa ni ya unyonge zaidi. Bali kadiri kazi ilivyo ya unyonge na kunyenyekesha mbele ya macho ya wanadamu, kadiri ilivyo ya kujificha, kuchokesha, kadiri ilivyo ya heshima ndogo, ndivyo haswa mnapaswa kuipenda zaidi, kama mnayo roho ya kimaskini. 16

Fanyeni kazi kwa bidii kwa ajili ya Mungu! Kazi zenu zinasaidia kwa kuwatunza mayatima wetu. Tukumbuke kile alichosema Bwana: "Kila wakati mlivyomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo mlinitendea mimi" (Mt.25:40). Je, wazo ambalo, tukifanya kazi ili kuwatunza mayatima wetu, tunaifanya kwa ajili ya Yesu mwenyewe, labda haituamshi zaidi na kutupa nguvu daima kuwa wenye bidii zaidi na kujitoa bila mipaka kwa kazi yetu?

Napenda kuwaona, watoto wangu wapendwa, katika umaskini na katika kazi, hata kama ni ngumu na ya kuchosha.

Wapendwa watoto, nawaomba na nawasihi wale niwafahamuo na ambao mimi mwenyewe nimewalea, na wale nisiowafahamu kwa sababu wataingia katika Shirika baada ya kifo changu, lakini niwapendao kama ningeliwafahamu: pendeni umaskini, utamanini umaskini! Mimi kutoka juu nitasali ili kamwe katika nyumba zetu kusiingiwe na utajiri, unadhifu, fahari, starehe. Hapana, hapana! Tuko maskini na tubaki maskini.

Kumbukeni kwamba ni afadhali kuhitaji kidogo kuliko kuhitaji zaidi. "Mungu wangu na yote yangu":huu ni utajiri wetu