WOSIA


III.

AGIZO LA TATU

UPENDO WA KINDUGU

           

Baada ya kuweka Ekaristia, Mkombozi alisema kwa Mitume wake tukifuatia sisi: "Nawapeni amri mpya: pendaneni; pendaneni kama mimi nilivyowapenda ninyi. Mkipendana, watu wote watajua kwamba ninyi ni wanafunzi wangu" (Yoh.13: 34-35).

Watoto wangu, haya ni marudio ya maombi ya mzee mama yenu: tafakarini mara kwa mara, haya maneno ili muweze kuyatimiza katika maisha na katika upendo wa kindugu. Kama mkiwa wanyenyekevu na wakimya mkiufuata mfano wa Moyo Mtukufu, hamtapata shida yoyote katika kutimiza amri hii ya upendo. Tafakarini ule mfano ajabu wa upendo, ambao ni Yesu! Pendaneni wenyewe kwa wenyewe kama Yesu alivyotupenda. Tafakarini upendo wa Yesu kwetu! Ni zipi tabia zake? Ni hizi: wema usio na mwisho, sadaka hadi kifo na kifo cha msalaba.

Kwa hiyo: wema kwa mitume, kwa watu waliomzunguka, kwa watoto waliokuwa wakitafuta kubembelezwa nae, kwa wenye dhambi, na hata kwa watesaji na wauaji wake mwenyewe.

Kwa wema mwingi alizungumza nao, aliweza kuvumilia udhaifu wao, aliwasaidia, aliwategemeza, aliwaponya na kuwasamehe. Na sisi je?

Kuweni wema, watoto wangu, yaani wakunjufu kwa wote. Kutaneni daima kwa ukarimu, kwa tabasamu la upendo, kwa neno zuri mdomoni. Furahini wakati mnapoweza kuwatumikia ndugu zenu, hata kama kufanya hivi itawagharimu kazi kubwa zaidi au shida. Hamwelewi ni furaha kiasi gani 12

mnayowapatia wengine kwa tabasamu la kirafiki, kwa neno moja zuri! Msiwahukumu wengine na kama hamwezi kukitetea kitu, acheni kuhukumu, ni Mungu ndiye anayefahamu nia ya mtu. mwangalieni kila mmoja kwa jicho jeupe la upendo na kwa hiyo mtaona yote kwa mwangaza mwema.

Kumbukeni mambo mawili: wema unafahamu daima kushukuru kwa ukunjufu hata kwa mambo madogo madogo; wema unafahamu kupokea kukubali misaada midogo ya kitu chochote anachofanyiwa, hata kama hazisaidii, kwa ukarimu na kwa kushukuru. Ishini daima katika amani na upendo kwa wote. Mungu aepushe mafarakano kati yenu. Waacheni wengine kwa hiari ili wawe na amani. Kuweni wema zaidi, kuweni wenye kujaa sadaka, utayari, kama Yesu kwa kuyatoa maisha yenu kwa ajili ya wengine.

Watoto wangu, Yesu ametoa maisha yake kwa ajili yetu: hatuwezi hata sisi kujitolea, kuacha furaha zetu, kwa jinsi tupendavyo sisi, ili kumfurahisha Yeye aliye katika wenzetu? Awali ya yote daima,wafikirieni wengine ili wajisikie vizuri, na baadaye mjifikirie wenyewe; na ingekuwa vema kama mkijisahau kabisa. Ishini kama Yesu kwa furaha ya wengine, na yawape nguvu maneno haya: "Kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi"(Mt.25,40).

Kwa hiyo mkiishi hasa kwa ajili ya furaha ya wenzenu, mtaishi kwa furaha na kuwa kitulizo cha Yesu, cha Moyo wake Mteswa. Wazo hilo lingeweza kuwatia moyo na kuwafanya muweke ahadi kila siku kwenye miguu ya msalaba: Moyo wa Yesu Mteswa, nataka kukupenda nikitoa furaha kwa wenzangu.

Ni shida labda kueneza furaha kati yetu? Hapana! Inatosha tu kuwa na moyo uliojaa upendo, tabasamu la kirafiki usoni, neno la upole mdomoni, kuwa tayari hata kwenye huduma ndogo za upendo zilizoangazwa kwa furaha takatifu. Mtakuwa hivi 13

malaika wa furaha, mionzi ya jua kwa Shirika letu lote.

Ishini watoto wangu, kwa ajili ya furaha ya wengine na kwa kuutuliza Moyo wa Yesu Mteswa. Kama mkijaribu hivi, kimya kimya, katika upendo wa kindugu, mtapata nguvu za upendo ambazo zitawapatieni uwezo wa kutoa sadaka kubwa, kama Bwana, siku moja atawahitaji.

Watoto wangu wapenzi pendaneni! Uwe mbali nanyi utengano, wivu ambao ni adui wa upendo, ubinafsi ambao unamfanya mtu ajifikirie yeye tu na awasahau wengine, tamaa inayofanya "umimi" uwe sanamu, jicho baya linalouona ubaya katika wenzake badala ya kuugundua katika yeye mwenyewe. Pendaneni wanangu wapendwa, ili mimi nikiwangalia toka ule ulimwengu mwingine, niwaone mmeunganika kwa upendo safi zaidi ili muweze kuunda moyo mmoja na roho moja. Hili ni agizo la motomoto, la mzee Mama yenu ambaye anawapenda toka ndani ya moyo.