WOSIA
XVIII.
AGIZO LA KUMI NA NANE NA LA MWISHO
KUVUMILIA HADI MWISHO
"Atakayevumilia hadi mwisho ataokoka" (Mt.10,22), asema Bwana. Kitu cha maana zaidi kwa maisha ya ndani ni uvumilivu. Wengi huanza kwa juhudi na bidii, wakitamani kwa bidii kubwa. Lakini hawafaulu haraka, wanakufa moyo, wanaacha kazi kwa kujidai kwamba hawafikii kufanya chochote, kwa hiyo haina maana ya kuendelea. Maskini! Uvivu na kiburi vinawafanya ili wasiendelee mbele. Huku ni kujitoa kwa kujisamehesha na kujifurahisha ili kuacha yote.
Kumbukeni, wanangu, maisha yetu ni mashindano, kushindana hadi mwisho. Hata askari ambaye tangu mwanzo alilazimika kurudi nyuma, lakini akiweza kumshinda adui na kumwangusha dakika ya mwisho, ameshinda na anastahili kusifiwa na kupewa zawadi. Tusiseme kamwe kwamba haina maana kushindana. Kupigana na kuvumilia katika mashindano ndicho kinachomfurahisha Mungu.
Isingekuwa shida kuwa watakatifu kama kila kujilazimisha kwetu kudogo kungeendelea hadi ushindi wa mwisho. Wakati mwingine Mungu anapenda huu uvumilivu ambao haurudi nyuma katika vita, bali hufanya upya kila siku kwa amani na utulivu, na husubiri hadi Mungu atoe ushindi. Niaminini, unyenyekevu ungekuwa wa kukabili vishawishi vikubwa, kama wema ungepatikana bila kuchoka na bila kushindana. Nakubali kuwa daima ni shida kuendelea kuanguka katika makosa yale yale. Lakini aminini, pia kuwa Mungu anapendelea zaidi shindano la uvumilivu, hata kama ni la kuchokesha sana, kuliko ule ushindi wa rahisi na wa muda mfupi.
53Watoto wangu, iweni basi na uvumilivu katika maazimio yenu, wavumilivu katika majaribio ya kuwa wema, wavumilivu katika majaribio ya kuwa na huruma na wavumilivu katika kufanya sadaka ndogo ndogo.
Wakati mmoja aliulizwa Mt. Yohani Berchmans, ni kwa jinsi gani inawezekana kumfurahisha Maria Mtakatifu. Yeye alijibu: "Hata kwa jaribio dogo la wema au la huruma, lakini lililofanywa kwa uvumilivu".
Mara ngapi inatokea mtu fulani, katika muda wa bidii na umoto moto moyoni, anafanya maazimio makubwa, na anakuwa mwaminifu kwa siku chache, baadaye moto unazimika, maazimio yanasahaulika, baada ya wiki mbili au tatu yote yanaanguka na kusahauliwa. Au mtu fulani anaazimia kufanya jaribio la aina moja la kuwa mwema, kupata wema, kwa mfano katika kurudia mara kwa mara wazo jema na anajaribu kwa siku chache, anashindwa, haoni maendeleo na anaacha yote. „Siwezi, haina maana mimi kujilazimisha"
Ina maana, mwanangu, ina maana. Haswa kwa sababu wewe unajitahidi bila kukata tamaa kwa sababu ya kutoona matokeo uliyotamani, unaufurahisha Moyo mtukufu. Jinsi utakavyoomba kwa muda mrefu, vivyo hivyo utapewa kwa kipimo kikubwa
Wanangu wapendwa, kutokana na ukosefu wa uvumilivu katika sala zetu tunakosa neema za kiroho. Tunahitaji neema nyingi ili kuufikia utakatifu, lakini tunaomba angalau ombi moja pasipo kuchoka? Mara kwa mara inatokea kwamba tunaomba kutokana na msukumo wa wakati ule: mara hii moyo wa kusali, wakati mwingine upendo wa Mungu, wakati mwingine tena kuwa na imani kutokana na hicho kinachotujia akilini. Na kwa kuendelea hatuombi tena neema za kiroho kwa sababu tuna mivuto ya mambo ya kidunia ambayo yanatuhusu zaidi. Oh kama tungeweza kujenga wazo lililo wazi la kuhitaji fadhila hii au ile, na tungefanya bidii katika kuipata! Kama
54tungesali vizuri na kuvumilia katika sala hii ya kusihi na kuomba, daima jambo lile lile, hata kama ni kwa miaka mingi, kwa ukweli, baada ya hii miaka ya uvumilivu, Mungu atatukubalia na atatupatia kutokana na kipimo kile kile tumwombacho. Lakini sisi hatuna huu uvumilivu kwa hiyo, hatupewi kile tuombacho kwa sababu ukosefu wa uvumilivu unakuwa hivi kwa kuwa hatuelewi kwa kweli kile tunachohitaji. Mara hiki, mara nyingine kile, lakini hakuna cha maana.
Kuweni wavumilivu wanangu! Kwa haraka uvumilivu utawapelekeni katika ushindi. Msiuache kamwe, kamwe msitake kufa moyo. Usijali, hata kama siku moja utaanguka mara mia, jambo la muhimu ni kwamba mara mia utainuka na kufuata njia iliyonyooka kwa utulivu na kwa imani.
Anza upya kila siku! Sio lazima kwamba wewe uone maendeleo, isipokuwa tu wewe ukiwa na nia njema: Hiyo inakutosha.
Ukiwa na nia njema, imani na uvumilivu utaelekea mbinguni! Kwa uvumilivu utaupata kweli Moyo