WOSIA
XVII.
AGIZO LA KUMI NA SABA
UPENDO NA HESHIMA KWA MASHIRIKA
YOTE YA KITAWA
Inaonywa mara kwa mara katika mashirika ya kitawa ambayo huwa na ugomvi kati yao. Hiyo inawakwaza walei na kutoa sifa mbaya kwa mashirika. Sio kazi yangu hapa kutafuta sababu hizi za kutoelewana. Mara nyingi inatokea katika pande zote mbili, ingawa mapenzi mema, kwamba ipo bidii ya juu zaidi inayoogopa kwamba kivuli kinaweza kuwa juu ya kazi zao.
Na wanasahau kwamba kazi kwa ajili ya Mungu ni nyingi ukilinganisha na kazi za Mungu zisizo na mwisho, na namba za mashirika ya kitawa mara mia zaidi ya sasa, yanaweza kufanya kazi kwa utulivu bila kuingiliana yenyewe.
Watoto wangu, ningependelea muwe na moyo ulio wazi kwa kila Shirika la kitawa. Kwa sababu kila moja limeundwa na watu waliojitakatifuza kwa Mungu na wanaojitolea katika sala, katika sadaka na katika kazi kwa ajili Yake. Utaachaje kuwapenda watu hawa, utaachaje kuwaheshimu!
Kiwe mbali nanyi kila kivuli cha wivu wa maendeleo yao. Maendeleo yao ni maendeleo kwa ajili ya kazi ya Mungu. Sio hicho tunacho kitamani hata sisi? Kwa kweli tunajitakia heri kwa maendeleo ya kazi yetu, sio kwa sababu ni yetu, bali kwa sababu tunafanya kazi hiyo kwa ajili ya Yesu. Tunatamani kwa hiyo maendeleo ya kazi yetu, kwa sababu yenyewe ni ya Yesu. Hayo maendeleo tunapaswa kuyatamani hata katika kazi za mashirika mengine.
Tunapaswa kumpenda na kumheshimu Yesu katika masista wa Shirika letu, wao ndio walio karibu zaidi na sisi,
50hiyo ni kweli. Lakini Bwana akituweka karibu na masista wa Shirika lingine, tunapaswa pia kumpenda na kumheshimu katika wao.
Tukumbuke tena kwamba unyenyekevu ni msingi wa wema wa Shirika letu, ambalo lilianzishwa kwa ajili ya wadogo na maskini. Vazi letu ni la kimaskini na rahisi. Katiba yetu inatuwajibisha kutoa nafasi ya kwanza kwa masista wanaovaa shela. kwa hiyo tupende kujiona wadogo zaidi, wa mwisho na wadhaifu kuliko mashirika mengine yote. Na hiyo ni nzuri kwa maskini kama sisi. Tusiwaonee wivu wale ambao Mungu amewapatia kazi za maana zaidi. Tunyenyekee katika ukubwa wa udogo wetu na tufurahi kwamba Yesu anapenda kutuona katika kazi rahisi zaidi na zisizo za maana sababu hata hizo hatustahili. Nafasi ya mwisho kwetu sisi ni ya uhakika zaidi. Tuishike kwa upendo, watoto wangu wapenzi.
Kamwe msiongee vibaya kuhusu Shirika lingine, kwanza, kama inawezekana, funikeni matendo yao ya udhaifu. Zungumzeni juu yao yale ambayo ni mazuri, wasaidieni wakati inapowezekana kama wanahitaji. Jitoleeni sadaka kwa ajili yao. Chochote kile mfanyacho kwa watu waliojiweka wakfu kwa Mungu, ambao ni mali yake, mnafanya kwa Yesu mwenyewe.
Pendeni haswa Shirika lenu kwa sababu Yesu amelichagua kwa ajili yenu. Ni familia yenu. Katika lenyewe mnapaswa kutakatifuzwa. Lenyewe linapaswa kuwaongoza njia ya mbinguni; kwa njia ya umaskini wake, njia ya kazi zake, lenyewe linapenda kuwapelekeni katika unyenyekevu mtakatifu. Lipendeni, kama mtoto mwema ampendavyo mama yake, bali hiyo haiwazuii kupenda kwa ukweli mashirika mengine ya kitawa.
Shirika letu kwetu sisi ni mama, mashirika mengine na ukasisi ni kaka na dada zetu. Watoto wema, wakipenda kumpendeza mama yao, wanapendana wenyewe kwa wenyewe
51na wanaishi kwa umoja na upendo. Na sisi, tukipenda kuwa kitulizo kwa mama yetu ambaye ni Shirika, tuishi kwa umoja kama kaka zetu na dada zetu, yaani ukasisi na mashirika mengine. Tufurahie maendeleo yao, utakatifu wao, sifa zao, tusikitike pamoja nao katika masikitiko. Tuwaendeleze, tuwasaidie inapowezekana. Hiyo itatupatia baraka na neema tukufu, na itakuwa kwetu sisi uthibitisho ambao hatuutafuti sisi wenyewe, bali utukufu wa Mungu, kwa ajili ya manufaa ya Kanisa na ukombozi wa roho.