WOSIA


XVI.

AGIZO LA KUMI NA SITA

BIDII KWA AJILI YA UKOMBOZI WA MIOYO

 

          

Mu-Ursula wa Moyo wa Yesu Mteswa anapaswa kusikia maombi ya uchungu yatokayo katika kinywa cha Bwana ambaye anateseka juu ya msalaba: "Sitio". Ni mlio wa uchungu utokao katika moyo uliojaa mateso akiona kikundi kidogo cha watu wanaofahamu kutumia nafasi ya kupata neema ambazo Yesu kwa mateso na kifo chake, ametustahilia sisi na vizazi vyote vya binadamu

Yesu ana kiu, na kiu hiyo ni kubwa hivi kwamba Yeye, ambaye kamwe hakulalamika, hawezi kuizuia hii huzuni. Anatamani watu wenye uwezo wa kumpenda na kuwapa wao badala ya upendo wao, hazina za neema zake, kwa kuwapeleka katika furaha ya umilele, mbinguni, pale ambapo anapenda kuandaa mahali kwa ajili yao.

Watoto wangu, uwake katika mioyo yenu, kwa mfululizo moto wa upendo kwa ajili ya roho. Ziokoeni, zipelekeni kwa Yesu, wafahamisheni watu, ukubwa wa wema wa Moyo wake: hili ndilo wazo ambalo tunapaswa kujifunga nalo. Kwa sababu Padri mtakatifu anaweza kufanya mengi sana kwa ajili ya kuziokoa roho; salini basi kwa ajili ya mapadri ili Bwana atume wafanya kazi katika shamba lake.

Msijizuie kufanya sadaka ndogo ndogo kwa nia hii: Kwa mfano msiwe na tamaa ya kutamani makuu, heshima au uvivu. Kuweni wenye moyo wa ukarimu wa kujitolea sadaka kwa hawa mapadri wetu wadogo, "in spe"(waseminaristi). Ni neema kiasi gani anaweza kuomba kwa ajili ya mapadri sista ambaye kwa ukimya, hafahamiki na ulimwengu, anajitolea kwa kazi rahisi na zisizo tambulikana, anafanya kazi, anajitoa 47

sadaka, anaweza kuvumilia kimya misalaba midogo ya maisha, na kwa kazi hiyo ya uchovu na kujitolea sadaka, Bwana anatoa neema kwa ajili ya mapadri. Siku moja katika hukumu ya mwisho yeye ataona matunda ya ukimya wake, kutofahamika na ulimwengu kwa ajili ya ukombozi wa mioyo, kwa ajili ya ile sadaka ya "u mimi" ya kupata neema na utakatifu kwa ajili ya mapadri. Wanangu, hili ni wazo la kushangaza! Na kama tunalo mbele yetu wazo kubwa, ni rahisi zaidi kufanya kazi na tuko tayari zaidi kufanya kile ambacho maumbile yetu hayapendelei.

Wakati nilipomtembelea Baba Mtakatifu Pio XI, kwa mara ya kwanza akiwa Balozi wa Baba Mtakatifu wa Warsavia, yeye alinifanya nitafiti kwamba Bwana Yesu hakuomba kitu kingine cho chote zaidi ya kusititiza sana kusali, ili kupata mapadri wema. Kwa mara ya kwanza nilipopiga magoti kwenye kaburi la Mt. Pio X, Baba wa Shirika letu, mama mmoja mfaransa, nisiye mfahamu, alinipa ile sala ya kuwaombea mapadri ambayo tunaisema kila siku. Sio labda kwamba hizi ni ishara wazi za mapenzi ya Mungu? Yesu hajionyeshi kwetu kupitia wasaidizi wake duniani ili kusudi tusali kwa namna ya pekee kwa ajili ya kupata mapadri wema?

Kwa uhodari basi, wanangu wapenzi, kwa vitendo, kwa uhodari! Unapaswa kuwa sadaka ile ambayo kimya kimya na kwa mfulilizo unatumika katika kazi, katika sala, na katika kuteseka, kwa ajili ya kuomba neema kwa ajili ya mapadri. Kila msalaba utakuwa mwepesi, kila maumivu yatakuwa mepesi, kila sadaka itakuwa nzuri zaidi kama vitapewa nguvu na ombi hili: "Yesu pokea toleo hili ambalo linakulilia mbinguni: Bwana tupatie mapadri wema na watakatifu". Waheshimuni mapadri, kamwe msiongee vibaya juu yao, hata kama wasipotenda vizuri, isipokuwa tu kama kuna umuhimu na ulazima wa kufanya hivyo.

Msizungumze kati yenu, juu ya mapadri, au 48

waungamishaji, bali watoleeni kwa Bwana daima kwa heshima kubwa. Kwa vikwazo ambavyo kwa bahati mbaya, wakati mwingine vinaweza kutokea kwa mapadri, ombeni msamaha kwa Mungu kwa nguvu zenu zote na jaribuni kuufariji Moyo wa Yesu Mteswa kwa sababu ya majeraha ambayo yanatokana na kutoneshwa na wale ambao wamechaguliwa kwa heshima kuwa mapadri.

Dada zangu, watoto wangu, msifikiri sana juu ya mateso yenu, ambayo wakati mwingine ni ya kubuni, kwa misalaba yenu midogo ambayo kwa upendo binafasi mnaikuza na hivyo hamwezi kuuona Moyo wa Yesu Mteswa, ulioingia katika uchungu kwa kutoamini kwa watumishi wake.

Utukufu wa matendo matukufu ni kushirikiana ili kuziokoa roho. Mimi ninaona kwamba utukufu wa zaidi ni ule wa ushirikiano kwa ajili ya utakatifu wa mapadri, na kwa uongezekaji wa wito wa kipadri. Kwa hiyo wekeni upendo na sadaka katika kazi hii ya maana! Katika kazi hiyo msichoke au kufa moyo, hata kama hamuoni hapa duniani matunda ya uchovu wenu. Ni afadhali zaidi! Yesu mwenyewe anakusanya matunda ya sadaka zenu.

Wewe maskini dadangu, uliyefikiri kuwa usiyefaa mtumishi wa Bwana, utaona mbinguni matunda ya kazi yako, ambayo Yesu atakulipia kwa upendo wake, na atakufurahisha kwa kukuonesha roho ambazo umezipata, kwa njia ya kazi, sadaka na kujitolea kwako, neema na mwanga, wa kutimiza zaidi kwa uaminifu wajibu huu mtakatifu wa