WOSIA


XV.

AGIZO LA KUMI NA TANO

UKWELI KWA WAKUBWA

 

           

Kuweni wakweli wanangu, jinsi mtakavyokuwa wakweli mbele ya wakubwa wenu, ndivyo zaidi mtakavyokuwa wema. Kanisa linawakataza wakubwa -na hiyo ni haki- kuingia kwa nguvu katika siri ya mioyo ya masista waliokabidhiwa. Wala kwa maswali, wala kwa kuogofya, wala kwa mvuto ambao wao watalazimika kufungua ufahamu wao wa nafsi. Lakini kila sista anayo haki ya kujiaminisha kwa sista mkubwa wake, na kumfahamisha kile kilicho chema na kibaya, kilichomo ndani yake, kwa sababu ni kwa njia hii sista mkubwa anaweza kumsaidia, na kumwongoza. Na huu uongozi wa mkubwa ni kwa ajili ya roho kama egemeo kwa mti dhaifu ambao, kila ukija upepo unakunjika.

Ukweli sio fadhila kwa ajili ya vijana tu, wale wanaoanza maisha ya kitawa, bali hata kwa wale walio wazee. Katika maisha ya kiroho, tunapaswa kuwa kama watoto, na watoto wanahitaji mkono wa kimama. Usiseme: "Ninae muungamishi kwa hiyo ananitosha". Ni kweli muungamishi mwema ni hazina ya roho, walakini nakueleza kitu kimoja, Muungamishaji anakufahamu tu wakati wa kuungama. Lakini una hakika kuwa unajieleza kwa ukweli? Si kwa sababu unapenda kumdanganya, hapana; bali kwa upendo wako mwenyewe, kujipendelea kwako kunakufanya kipofu. Wewe mwenyewe hujifahamu vizuri, bali mkubwa wako anakufahamu zaidi kwa sababu anaona vile vitendo vya udhaifu ambavyo wewe huvioni.

Angeweza kwa wakati mwingine kukuepusha na mabaya, lakini hawezi kwa sababu wewe unakaa mbali naye, 44

huna imani naye, hupendi kwamba „aingilie" maisha yako ya ndani. Dada zangu, niaminini, muungamishi anafikiri mara nyingine kwamba, yule anayeungama ni mtakatifu na ni sadaka ya upendo, ambavyo mkubwa wako, lazima kwa bahati mbaya afikiri tofauti. Muungamishaji anasikia maneno tu, bali mkubwa wako anaona matendo.

Ukweli hauna maana kwamba unapaswa kuongea kila dakika na Mkubwa wako, kumweleza maisha ya roho yako, kujipendelea kwa nafsi yako mwenyewe; Hapana! Mimi namwita mkweli yule ambaye hafanyi au hasemi chochote ambacho hakifahamiki na mkubwa wake. Ambae anahisi daima kwamba mkubwa wake anafahamu kila kitu anachofanya, anachoongea, hadi anachofikiri. Na kwamba hamwahidi yeyote kutosema chochote kwa mkubwa. Kamwe! Inawezekana kuwa mkweli sana mbele ya wakubwa, yule ambaye mara chache anaongea kuhusu maisha yake ya kiroho. Na anaweza kukosa kuwa mkweli yule ambaye anang'ang'ania, anamsumbua mkubwa kwa mazungumzo, kwa sababu anaongea kile tu kimpendezacho, na anaficha kile ambacho hapendi kusema.

Nakushauri mtoto wangu, mfahamishe mkubwa wako juu ya fadhila gani haswa unayoifanyia kazi; sio kwa sababu lazima akushauri yeye, hayo ni juu yako, bali wewe mweleze ili afahamu ni juu ya nini haswa unafanya kazi, na wakati mwingine yeye aweza kukusaidia. Mjulishe mara kwa mara angalau kila baada ya miezi mitatu, kuhusu utafiti wa maisha yako na utakuwa na msaada mkubwa wa kuendelea katika kazi hiyo.

Omba wakati mwingine akuambie yale yote anayoyaona kwako yasiyo kamili, mapungufu, na akushauri mwenendo mwema ili urekebishe kile ambacho hakiendi sawa sawa. Acha uongozwe na mkubwa. Yeye ni egemeo ambalo Mungu mwenyewe amekupatia kwa ajili ya roho yako. Usiangalie 45