WOSIA


XIII.

AGIZO LA KUMI NA TATU

EKARISTI TAKATIFU

 

       

Wanangu wapendwa, Yesu katika Tabernakulo ni jua la maisha yetu, utajiri wetu, furaha yetu na kila kitu chetu duniani.

Furaha ya mtawa ipo kwenye mapenzi ya Mungu na katika Ekaristia Takatifu. Ukitimiza kwa uaminifu mapenzi ya Mungu itakuwa vyema kukaa mbele ya Tabernakulo! Yesu akiona unatimiza mapenzi yake atakupenda, atakuja kwako atakaa katika moyo wako uliounganika kabisa na mapenzi yake na unaweza kusema hivi: "Sio mimi ninaye ishi tena bali ni Kristo anaishi ndani yangu" (Gal. 2,20).

Mpendeni Yesu katika Tabernakulo! Pale ibaki daima mioyo yenu, hata kama kimwili mko kazini. Pale yupo Yesu, ambaye twapaswa kumpenda kwa umoto moto na kwa moyo wote. Kama hatufahamu jinsi ya kumpenda, angalau tutamani kumpenda daima zaidi. Komunyo takatifu iwe ni kiini kati yetu ambacho kinatuunganisha kila siku kwa maisha yetu yote. Wakati wa maana zaidi katika siku ni ule wakati wa komunyo takatifu, wakati ambao Mungu wetu na Bwana anakuja upya kutumiliki katika mioyo yetu maskini.

Tujifungue kabisa kwa Bwana wetu mkubwa, tuwe huru kwa kila tamaa zote za duniani, kwa kuhukumu, kwa kutamani makuu, wasiwasi na mawazo ya kidunia. Yote ndani yenu yawe kimya, aongee Bwana. Bwana alinde, Bwana atawale, Yeye tu aishi ndani yenu. Jishikeni kwa Yesu kama Maria Magdalena alipokuwa kwenye miguu yake. Sahauni yote katika ule wakati mpendelevu, wa kuwepo na Yesu na ombeni, ombeni kwa moyo wa bidii, kwa bidii na hata kwa kusisitiza: "Yesu nipatie upendo daima mkubwa zaidi". Yeye kwa kweli alisema: 39

"Ombeni mtapewa" (Mt.7,7). Ombeni basi, mkiwa na uhakika kuwa Yesu atawasikiliza.

Moyo wenu tangu asubuhi hadi jioni, uelekee tabernakulo. Jaribuni! Hii tabia inapaswa kushinda, na inawezekana kuipata na kujiunga nayo. Unaweza kuisalimu Sakramenti kiroho, hata kama kimwili uko mbali, uko kazini. Wakati inapowezekana nenda na amkia mara moja, mara mbili au zaidi fanya kulingana na nafasi inavyoruhusu. Nenda kwa Yesu kama mtoto kwa mama, kama rafiki mwenye huzuni na mchovu kwa rafiki yake, ambapo ndipo kiini cha kupata kitulizo na msaada.

Nenda na mwambie Yesu wako chochote kile kilichomo moyoni. Wewe humwoni, bali Yeye yuko pale katika tabernakulo. Hivi unaweza kuamini hata zaidi ya kuweko kwako. Na wakati unapiga magoti mbele ya tabernakulo na huelewi ufikiri nini, au unapoteza mawazo, nyenyekea kabisa kwa undani, kadiri uwezavyo. Wewe uko pale kama kitambaa cha nguo ambayo haijasafishwa, na huwezi chochote, bali jitoe wazi kimya kimya, kwa unyenyekevu, umaskini wako kwenye kitendo cha mionzi ya upendo ambayo inatoka kwenye tabernakulo. Ni kama jua linavyofanya nguo kuwa nyeupe, vivyo hivyo Yesu ataifanya mioyo yenu maskini myeupe na mizuri.

"Hata kama makosa yako yanakuogopesha,

hata kama unajisikia kuchoka katika kumtumikia Yesu,

Yeye jua lako atakuokoa, Yeye anafanya kazi kwa ajili yako,

ili wewe ujiweke wazi kwake kwa kitendo cha mionzi yake".

Baki katika ukimya, jitokeze kuelekea kwenye mionzi ya Jua lako la Ekaristia. Hata kama unajiona hukufanya lolote, ngojea na uwe na imani. Yesu mwenyewe anafanya kazi katika roho yako. Usimkimbie!. 40

Na kwa wakati mwingine mtoto wangu, uchungu, mahangaiko na kufa moyo, vinapenya ndani ya moyo wako, jaribu kuviondoa, haswa kwa kwenda kwenye tabernakulo. Pale ndipo kwenye hazina yako.

Zinawezaje kutudhuru shida hizi na maudhi? Zenyewe haziwezi kutuondolea Yesu, na mpaka tuwe na Yesu ndipo tutakuwa na furaha ya mbingu katika Yeye, mwanga wa mbingu, na mbingu yenyewe. Chochote kile cha duniani kitakuwa kidogo sana mbele ya huu ukweli!. Na baadaye, wakati unapokuwa umepiga magoti mbele ya tabernakulo, fungua kabisa moyo wako, kwa huo upendo, na uwe na hakika kuwa Yesu atakubali tamaa yako, hata kama wewe unajisikia umepoa na wa baridi. Yeye atakusaidia kufikia ule upendo ambao kwa moyo wako wote unautamani.

Yeye atabadili upendo wako usio kamili na dhaifu na atakupa upendo ule mkubwa wa Moyo wake Mtukufu. Na wewe, mdogo, maskini, usiye kamili, "mdudu mdogo" utapendwa na Yesu wako, Mwokozi wako, Mungu wako, na unaweza kusema kwa hakika: "Yesu ananipenda".

Ni mwema kiasi gani Yesu wetu! Mpendeni katika Sakramenti ya upendo! Yeye ni hazina yenu. Ishini kwa ajili yake. Kwa Yeye jishikeni wakati wa giza. Yesu awe taa yenu wakati wote wa maisha yenu ya kitawa, na siku moja juu katika umilele.