WOSIA


XII.

AGIZO LA KUMI NA MBILI

UTULIVU WA ROHO

 

       

Mmoja wa wakubwa wa waandishi wa vitabu vya maisha ya kiroho aliandika kwamba, kuwa daima na utulivu moyoni ni kitubio kikubwa sana. Na ni kweli, kwa sababu inahitaji nguvu nyingi za kujitoa ili kujitawala mwenyewe, kujihinisha, kuwa daima mtulivu, kama nuru, mwenye furaha, mtulivu japo una shida, ujisikiapo mgonjwa, wasi wasi, ukiwa na taabu. Utulivu wa rohoni na furaha ya ndani ni msaada mkubwa sana kwa kazi ya kiroho. Kwa roho ni sawa kama vile ambavyo jua lilivyo muhimu kwa ardhi. Kama ilivyo kwenye kitendo cha mionzi ya jua maua yanachanua na matunda yanakomaa, vivyo hivyo katika moyo uliotulia, wenye furaha, unakuza ua zuri la utakatifu linalozaa matunda mengi ya wema.

Jua angani na moyo wenye furaha duniani, ni furaha kiasi gani wanatoa kwa wanadamu, na ni kitulizo kiasi gani kwa mioyo!

Kitendo kikubwa cha upendo kwa ndugu ni utulivu wa moyoni ambao daima unaeneza karibu nawe mwanga na joto. Mtu mwagavu na mwenye furaha, anapita kimya kama mionzi ya jua hata kama anaona uchungu kwamba hafanyi lolote jema - kwa sababu hajui kwamba ameamsha kwa utulivu wake tabasamu nyingi za wazi katika vinywa vya wengine, kwamba amemimina katika mioyo mingi faraja na kitulizo, kuwa amewasha moto katika mioyo iliyokuwa baridi, ameondoa mawingu ya giza, kwa wale wasio na matumaini na wamekata tamaa, pia bila kufahamu anaotesha furaha nyingi kando kando yake. Yeye hafahamu, bali Mungu anafahamu. Ni Mungu tu ndiye anampatia ustahimilifu huu wa furaha ambao yeye 36

anautoa kwa wengine.

Kwa kweli inahitaji nguvu nyingi za kiroho ili kuweza kushikilia huu mng'ao wa utulivu. Sio rahisi kuwa mwenye furaha, wakati ambapo mahangaiko yanatuchokesha, wakati watu wakituchosha na kutusumbua, wakati ulegevu wa kazi hautuachii nafasi ya kupumzika, wakati magonjwa yanatupunguzia nguvu na uchungu wa kimwili unatuumiza, wakati tunapojisikia kuanguka chini ya mzigo wa msalaba. Hapana sio rahisi! Yule tu anayeunganisha mapenzi yake na ya Mungu, ni yule tu anayetafuta furaha katika mapenzi ya Bwana aliye juu mbinguni ataweza kuhifadhi ndani yake huu utulivu mtakatifu, furaha hii yenye mwangaza usio wa kawaida, usio wa kidunia.

Mtoto wangu kama umeingia Shirikani kumtafuta Mungu, unapaswa kutafuta pia furaha kwa sababu hapa unayo chem chemi yenyewe ya furaha, unae Yesu kwenye Tabernakulo, Yesu katika komunyo ya kila siku. Umezungukwa na mapenzi ya Mungu. Umekosa nini tena kuwa na furaha?

Kama ungetambua na kuelewa hii furaha ya maisha ya kitawa, lazima utakuwa na furaha. Na furaha yako haitategemea mambo ya nje, itamulika kwa nje na kutia joto moyoni mwako. Na kwa namna hiyo utakuwa "mwangavu".

Mpende Yesu, mpende juu msalabani, mpende kwenye Tabernakulo, mpende katika mapenzi ya Mungu, na utakuwa daima mwenye furaha; na hii furaha itakugeuza kuwa jua kwa ajili ya wengine, na hata kwa Yesu ambae katika Tabernakulo amezungukwa na ubaridi na upweke. Hii siyo kazi ya ajabu?

Kumbuka kwamba mtu mwenye furaha, yeye mwenyewe ni mtume ambae bila kufahamu anainjilisha na kuwapeleka watu kwa Mungu, kwa sababu anaelezea kwa wanadamu pasipo maneno, bali kwa tabasamu angavu kwamba ni vema, vema sana kumtumikia Mungu na kwamba kumtumikia Mungu ni 37

kupata furaha na amani ambayo ulimwengu hauwezi kutupatia.

"Ee Bwana unijalie kuwa mionzi ya jua,

inayoeneza mahali popote faraja na furaha,

inayowatangazia watu wote utukufu wako na upendo,

pia ni kama tabasamu lako,

Ee Mungu wa milele!

Watoto wangu, iweni wenye furaha, waangavu, watulivu na mtaufurahisha Moyo wa Kristo; mtakuwa kitulizo kwa wakubwa wenu, kwa wenzenu, na kwa watu wote ambao mtaishi nao. Kilicho cha maana zaidi yatimizeni kwa furaha mapenzi ya Mungu ambaye, kama asemavyo Mtakatifu Paulo ni utakatifu wenu: "... haya ni mapenzi ya Mungu, kutakatifuzwa kwenu" (1 Ts.4,3). Kwa hiyo kuweni daima watulivu, wenye furaha twendeni kwa imani kumwuelekea M