WOSIA


I.

AGIZO LA KWANZA

 

UPENDO KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU

 

Jambo la kwanza na wosia wa shauku zaidi ambalo ninawaeleza watoto wangu ni hili: Pendeni, pendeni daima zaidi kwa moyo wa moto wa mapendo Moyo Mtukufu wa Yesu, kupitia Moyo Safi wa Bikira Maria.

Bwana ameniteua mimi, dhaifu, kuanzisha tawi hili jipya ambalo limetokana na shina la Wa-Ursula wa zamani, ambalo ni changa zaidi na dhaifu zaidi, la pekee na mali ya Moyo Mwema wa Yesu.

Kwa hiyo wajibu wetu mkubwa zaidi wanangu ni kuupenda huo Moyo Mtukufu kwa nguvu zetu zote.

Tuupendeni huo Moyo Mtukufu. Maisha yetu yote na yawe ni kuendelea kuupenda huo Moyo Mwema sana wa Yesu.

Ili muweze kuupenda, ombeni huu upendo.

Matamanio ya maombi yenu yawe katika sala hii (rehema ya siku 300). "Moyo Mtukufu wa Yesu nifanye nikupende daima zaidi".

Ombeni kwa ajili yenu wenyewe, na kwa kila sista, huo moto wa upendo na juhudi kwa Moyo wa Yesu. Upendo wenu kwa Moyo wa Yesu utawale mawazo yenu ili yaelekee daima zaidi kwake.

Kitu mkipendacho katika mawazo yenu kiwe ni Moyo Mtakatifu wa Yesu. Upendo kwake Yeye uamshe ndani ya mioyo yenu imani isiyotikisika katika wema wake, imani ya mtu ambaye, kwa amani ya ndani, anangojea yote toka kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Litokee lile litokealo: ninyi bakini katika ukweli wa heri ambao Moyo wa Yesu atawaongoza kwa njia njema hata kama imeoteshwa miiba. 6

Msipoteze kamwe utulivu wa moyo ambao umepumzika katika Moyo wa Kristo, wala imani ya kutikisika kwa maana yote yataendelea vizuri kwa sababu Yeye anaongoza kila kitu kwa mapenzi yake.

Hii imani isiyotikisika, ya kitoto na tulivu, ni mojawapo ya majaribu makubwa ya upendo ambao tunaweza kuyatoa kwa Yesu.

Iweni na imani, wanangu, kuweni na imani, hata kama upeo wa maisha ungekuwa mweusi kama usiku.

Kuweni na imani! Yesu, Moyo wake, umeshinda ulimwengu na udhaifu wake wote. "Msiogope, enyi kundi dogo, kwa sababu Baba yenu amependa kuwapa Ufalme wake". (Lc.12:32)

Ninyi ni sehemu ya ufalme wa Moyo wa Yesu, tafuteni kwa hiyo kitu kimoja tu; kuupanua huo ufalme, huo utawala wa Moyo wa Yesu katika mioyo na msihangaike na kitu kingine. Moyo wa Yesu unawapa chochote kile ambacho mnahitaji kwa ajili ya wokovu wenu. Hamhitaji kitu kingine chochote.

Tupatie ee Bwana, upendo, upendo ambao daima ni mkubwa zaidi na hiyo inatutosha.

Ningependa kuupenda kwa kweli ule Moyo Mtukufu kwa upendo ule ambao utakuwa kwake kitulizo, upendeni kupitia kwa Moyo Safi wa Maria, Nyota yetu angavu ya bahari, ambayo kwa nuru ya mionzi yake inatuelekeza katika Jua, kwa Moyo Mwema wa Yesu.

Wakati mioyo yenu ikiwa baridi na gizani, angalieni Nyota yetu, jishikeni kwa Moyo safi wa Maria, mwombeni huyu Mama yetu ili aweze kuangazia kwa mwanga wake, giza lenu, kwa kupasha joto mioyo yenu ili muweze kuupenda zaidi na zaidi Moyo Mtukufu wa Yesu.

Na mwisho mshuhudieni upendo wenu, kwa kufuata kwa uaminifu na kwa mfululizo fadhila zake. Mkizifuata

mtaonyesha kuwa watumishi wake waaminifu, watumishi wampendao kuliko vitu vyote.

Katika maagizo yafuatayo, napenda watoto wangu, kuweka mbele ya macho yenu fadhila za Moyo Mtukufu, nikiwaomba: wanangu, fuateni, fuateni kwa uhodari fadhila za Moyo wa Yesu, katika hizo ndipo kwenye upendo wenu, maisha yenu, utakatifu wenu na utukufu wenu wa milele.